Wazo la Biashara-Biashara ya Mtandao

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Wadau kwa muda sasa nimekuwa nikitaka kufanyia kazi hili wazo ila noana kila mara naliahirisha nafikiri na changamoto za maisha zinachangia pia.Wazo lenyewe ni hili:
Nimekuwa nikiona jinsi wajasiriamali mbalimbali wakihangaika kutafuta masoko ya bidhaa zao na hii inapelekea biashara zao kudoda ama kwa kukosa wateja au basi kwa kushindwa kuwafikia.Ili kutatua hii shida nikapata wazo moja:

Kwa kuwa SIDO wameshindwa kuwasaidia kwa kuwa na mfumo wa Quality Control yaani kudhibiti ubora wa bidhaa zao nikaona nichukue jukumu la kufanya hivyo yaani kudhibiti Ubora.Pili kwenye masoko nitatumia mfumo wa network Marketing kwa maana nyingine wajasiriamali hawatahangaika kufanya stocking bali watazalisha biashara zao kisha tunakuwa na mfumo wa marketing ambao utawalipa wajasiriamali vizuri na wale watakaonunua bidhaa zao na kuwashawishi wengine kununua pia watapata Commission.

Kwenye marketing sio shida sana maana systeme za kidigitali kuwezesha hilo tayari ipo kanahitajika kamtaji kadogo to then biashara iende.Panapo nipa shida na hapo kwenye Quality Control nimejaribu kufanya utafiti wa namna bora ya kusimamia ubora wa bidhaa za wajasiriamali lakini bado nimekwama.

Nimeleta uzi huu jamvini ili wanajamvi tushirikishane mawazo na kwa wale ambao tayari wana uwezo wa kutekeleza hii project na kuwekeza wanaweza kulifanyia kazi hili wazo.Jambo al msingi ni kutengeneza mfumo ambao utawawezesha watu kuwa producers of what they consume na consumers of what they produces.

Naomba kuwasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…