V Chief
Member
- Aug 20, 2023
- 78
- 145
Nimekaa na kuwaza ya kwamba kama inavyofanyika katika nchi zingine basi hata Tanzania inawezekana tukiwa na utayari na mpangilio mzuri wa mikakati katika nyanja mbalimbali za utoaji huduma.
Mfano, kwa mtu mwenye duka/biashara ya kuuza bidhaa zozote iwe simu, nguo n.k anaweza kufungua website ya duka au biashara yake na kuweka humo bidhaa zote zinazopatikana zikiwa na bei yake elekezi ambapo mtu anaweza kuchagua bidhaa hizo na kuzilipia popote pale alipo(hususani nyumbani) ambapo sio lazima afike dukani hapo na mwenye biashara akawa/akingia ubia na mtu ili awe anafanya delivery kwa wateja wake katika eneo husika la mji kwa kila mteja aliyenunua bidhaa kwa gharama nafuu kabisa(yawezekana 1000tshs) kumfikishia mteja mzigo kupitia mawasiliano aliyotoa na sehemu ambapo mteja huyo anapatikana.
Dhumuni langu la kuleta hili wazo kwenu wana JF ni kuweza kupata maoni ni kwa namna/kiasi gani ili wazo linaweza kufanikiwa na ni changamoto zipi ambazo unaona zinaweza kujitokeza kwenye utekelezaji wa suala hili.
Karibu kwa hoja zaidi, Ahsante.