Wazo la biashara hili hapa kwa wenye mitaji

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,637
Habari wakuu,

Twende moja kwa moja katika wazo.

Kutokana na maeneo mengi ya Tanzania kukosa huduma ya umeme mtambo huu wa mashine ya kunyolea na pia kuchaji simu ambao unaweza kuhamishika unaweza kuwa msaada wa kiuchumi kwa wajasiliamali.

*Mtambo huu unauwezo wa kunyoa watu 10-12 kwa ukubwa huu,

*Ukikosa wateja wa kunyoa utaweza kuchaji simu

*Unafaa kwa matumizi ya maeneo ambayo hayana umeme (Vijijini).

*Unatumia solar kama chanzo cha nguvu ya umeme,ndani yake kuna power bank inayotunza umeme.

*Kinyozi anaweza kusafiri na mtambo huu kwa kutumia baiskeli pikipiki au gari

*Mtambo unauwezo wa kutanua panel wakati wa kunyoa na kuficha panel zake wakati wa kusafirisha.

*Ukipata kijana mchangamfu unaweza kunyoa watu wengi kika siku.

*Mtambo una mita ya umeme ambayo inasoma matumizi hivyo unaweza kutafuta kijana na ukamuajili kwa ajili ya kazi hiyo na mkawa mnalipana kulingana na matumizi. (Atakua analipa kadri anavyo tumia).

*Unaweza ukawa na mitambo kama hii mingi kadri uwezavyo katika vijiji na maeneo mbalimbali.

*Gharama ya mtambo mmoja ni 500,000/-

*Inatumia mashine za kunyolea zile za umeme wa kawaida

WAZO LILIKUA HIVI.

Mtambo wa kunyoa au kuchaji simu ambao unahamishika kifata mikusanyiko ya watu mfano shule,vilabu na minada

Mtambo utumie nguvu ya jua.






ZIADA

Pia kwa wajasiliamali ambao wana mawazo ambayo yanahitaji tekinolojia ya umeme na electronics tunawakaribisha kuyafanya mawazo hayo kuwa kweli.

Gharama ya kubadili wazo kuwa uhalisia (mtambo au Kifaa ni kwa mtoa wazo mwenyewe).

Wasiliana na mbunifu wa mitambo 0629068815
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…