Wazo La Biashara-Online School

Wazo La Biashara-Online School

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu wadau;

Changamoto:
Leo naona niwashirikishe watu FURSA kidogo.Fursa hii sio mpya ila ni ya kipekee.Tunajua kwamba siku hizi mtandaoni kuna mambo mengi sana ambayo mtu anaweza kujifunza na akawa competent an kuingiza pesa.Hata hivyo mambo haya mengi hayajapangiliwa katika namna ambayo yanaweza kumfaa Mtanzania.Kwa mfano mafunzo mengi yako kwa Lugha ya Kiingereza na Lugha Nyingine.Pili Mafunzo mengi hayaakisi mazingira yetu.

Wazo:
Wazo ni kuanzisha chuo kinachotoa Mafunzo kwa njia ya Mtandao au kwa mfumo wa mseto(Hybrid).Mafunzo hayo yanaweza kuwa ya stadi na taaluma mbalimbali na yanweza kuwasaidia watu kufahamu kuhusu fursa ma kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.

Fursa:
Fursa ya kutengeneza Pesa iko katika kuuza access ya mafunzo hayo,kuuza vyeti kwa watakofaulu katika mafunzo hayo au kuuza live session na support.

Gharama
Gharama za kuanzisha mradi huu zitahusisha kuandaa maudhui ya kufundisha,kuandaa server na mfumo wa kutolea mafunzo,kutangaza mfumo ili ufahamike na wengi.

Changamoto

Changamoto ni ubora wa maudhui na ushindani kutoka katika watoa huduma wa kutoka nje na pia ushindani dhidi ya watoa mafunzo wanaofundisha live session

Je unafikiri hii fursa ina kufaa?Unaweza kuanza mdogo mdogo au ukajiunga na wengine kulinga na aina ya utaalamu mlio nao na kutengeneza timu ya kufanya kazi pamoja.

Ni wa zo tu na sio jipya ila bado lina FURSA
 
Mafunzo ya lugha ya Kiswahili online, sio kuandika wala kujua sijui nini. Kumfanya foreigner azungumze lugha kwa muda mfupi
 
Naona Wakenya ndio wanajihusisha sana na hii fursa. Ukiingia Youtube utakuta walimu wengi wanaofundisha kiswahili ni Wakenya. Labda kwakuwa wanakimudu vizuri kiingereza. Hivyo kufanya kuwa rahisi kufundisha kiwahili kwa kutumia kiingereza.
 
Mafunzo ya lugha ya Kiswahili online, sio kuandika wala kujua sijui nini. Kumfanya foreigner azungumze lugha kwa muda mfupi
Mkuu hio pia ni fursa ingawa muktadha wa wazo langu ulikuwa ni kwa ajili ya kuchangamasha soko la ndani zaidi.....
 
Back
Top Bottom