Wazo la biashara, ukiona yafaa lifanyie kazi

Wazo la biashara, ukiona yafaa lifanyie kazi

Ambition plus

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
6,101
Reaction score
11,381
Kwema?

Nakuletea wazo langu la biashara, ukiona lafaa chukua... Nunua kiwanja pembeni ya mji,mana huku wanapenda sehem zilizojificha,jipange jenga hata rooms 5,ila ukiweza kujenga room 20.

Kila room utachukua 20,000/=tsh per night. Ukiwa na rooms 5 utazidisha hapo,itakuwa ni laki kwa siku,usisahau huku rooms zinaanza kulaza kuanzia saa tatu,kabla ya hapo ni "show time tu" So ukipiga na show time utajua mwenyewe utapata ngapi... Tukirudi kwenye mahesabu hio laki ukipiga mara mwezi,utakua umekunja 3M,sasa hapo mahesabu ya show time sijayajumlishia,usisahau kuna malipo ya wafanyakazi na wenye serikal yao,umeme n.k...

Hii itakulipa kama utakaa mwenyewe ama utaweka mtu mwaminifu...

Haya twende ukiwa na rooms 20 kwa siku utapata laki 4,
Na kwa mwezi ukizidisha ni million 12...unataka nini tena,bado hapo mafichoni hujaweka vinywaji na chakula(usisahau nguruwe)

Atakuja mtu atasema mahesabu ya kwenye madaftari,sijui "motivation speaker "

Njoo ufanye research ujionee,siongei porojo

Local Guests house inalipa sana Unguja.
 
Hii inawafaa baadhi, maana hapo una-promote uzinzi huko mitaani. Kwa wasiojali hayo niliyotaja hakika ni fursa njema japo fanya mapato yake ni nusu ya hicho ulichotaja. Kuna siku utapata kama ulivyonena na siku nyingine utapata kidogo
 
Mkuu mimi nimewaletea fursa kazi kwenu kuitafakari kwa kina.
 
Haka ka biashara hua nakawaza sana. Naamini ni kabiashara ambako hakakulazi njaa na kanalipa kuliko kujenga nyumba za kupanga.

Kuhusu kuwa na mtu muaminifu ni ngumu, mi naona bora kuingia gharama kidogo unafunga cctv kamera.
 
Kuna mzee jirani yetu anasema kwa kujiamini kabisa 'nyumba za wageni zimesomeshea watoto'. Anadai tunachofanya uko yeye hajui anachojua ni kwamba alijenga wageni wapate mahala pa kupumzika. Anazo nne navyosikia na hazimpi stress hata kidogo. Last born wake ashamaliza chuo mzee anakula maisha tu
 
Haka ka biashara hua nakawaza sana. Naamini ni kabiashara ambako hakakulazi njaa na kanalipa kuliko kujenga nyumba za kupanga.

Kuhusu kuwa na mtu muaminifu ni ngumu, mi naona bora kuingia gharama kidogo unafunga cctv kamera.
Mkuu, baadhi ya wateja wakijua tu kuna Cct hata nje ya geti tu hawaji tena kwenye lodge yako
 
Utapigwa na kitu kizito hutaamini kabisa.

Nje ya mji mkoa gani?, mteja ni nani?, kitu gani kimshawishi mteja awaze kujamiiana?, utafungua bar?, hio itakuwa ni gesti au danguro?, kama ni gesti utalipia vibali ushaweka kwenye hesabu?
 
Huo mtaji wa kuwekeza mbali na mji ni changamoto.
Mkuu hebu rudia kusoma bandiko langu uelewe.
Unguja kupata kiwanja pemben kidogo ya mji sio gharama sana kama uko ufukweni na katikati ya mji...
 
Utapigwa na kitu kizito hutaamini kabisa.

Nje ya mji mkoa gani?, mteja ni nani?, kitu gani kimshawishi mteja awaze kujamiiana?, utafungua bar?, hio itakuwa ni gesti au danguro?, kama ni gesti utalipia vibali ushaweka kwenye hesabu?
Mkuu haujasoma bandiko langu vyema,rudia tena kusoma...
Unguja dini imetawala,wanapenda sehemu za mafichoni sana...
Kabla hujawekeza pesa yako kwenye biashara yeyote,fanya research kwanza...

Sijapoteza mda wangu kuandika,namaanisha...

Ndio mana nikasema ukiona "yafaa" si lazima akili kumkichwa.

Njoo nikutembeze uone mkuu,
Usafiri na kula nitakugharamia mimi.
 
Watanzania bara hawaruhusiwi kumiliki ardhi zanzibar ,ila kama unanunua kwa uwekezaji wa si chini ya dola 100,000 sawa na mil 260
 
Kama unaitaka pepo hii biashara ipitie mbali..
Ila kama unaitaka pesa,hii ndio biashara...
Njoo ufanye research utanishukuru baadae.

Humu kuna watu wa kila aina,
Wenye kumiliki biashara hizi watatupa mwongozo.
 
Back
Top Bottom