Wazo la Biashara Vs Mtaji

Wazo la Biashara Vs Mtaji

Che Robert

New Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
2
Reaction score
0
Habari wandugu,
Naomba mawazo yenu. Najaribu kuumiza kichwa jinsi ya kupata mtaji. Hivi sasa nimefanya utafiti na kujiridhisha kuhusu biashara ya Jumla ya Vinywaji Baridi. Frame ninayo tatizo mahali pa kupata mtaji wa km 8m mpaka 10m ili niwe na bidhaa za kila ujazo na za makampuni mbalimbali ukizingatia makampuni sasa bidhaa zao nyingi huhifadhiwa kwenye chupa za plastic.

Naomba ushauri najua kuna mabank lakini ni benki ipi ipo tayari kumsaidia mjasiriamali anayetaka kuanza bishara mpya.
Asante
 
Mkuu kabla yakuangalia mlango wa Benki, hebu jaribu kuongea na Mawakala wa vinywaji hivyo wakubwa na wakati, kama ikiwezekana washawishi juu ya kufanya ubia, yaani unanunua mzigo nusu kwa cash na nusu wakupe kwa dhamana. Hakikisha una nyaraka muhimu na eneo lako la biashara ni nyeti. Pia tengeneza mtandao wa wateja katika eneo husika. Nikutakie mwanzo mwema Mkuu.
 
Asante sana ndugu.
Wauzaji wakubwa wao huuza jumla kwa utafiti wangu ni kuwa wauzaji weengi hununua toka kiwandani kwa kuletewa na gari na sio toka kwa wauzaji wenzao wa jumla. Ukinunua toka kwa wenzako bei itakua kubwa sana.Nimepata jamaa anayesdambaza maeneo ya Tegeta wa Azam akanishauri kuwa na huo mtaji. Mali kauli hawana vinginevyo ufanye nao biashara ya thamani kubwa sana na uwe nao kipindi kirefu kwenye biashara.

Nakaribisha mawazo yenu wandugu.
 
tunashauri mtu kufanya biashara anayopenda, pia kumtia moyo ili angalau aanze biashara, kwani siyo vyote faida/pato au changamoto unaweza kuziona kabla ya kuingia uwanjani, pia tunasisitiza utafiti yakinifu wa kina kabla hasa masoko, gharama za uwendeshaji kwa kifupi SWOT analysis na mbinu zingine, mm nachojua aina hiyo biashara turnover ni kubwa sana tatizo ni profit margin inakuwa ndogo sana, unavyofikiria MKOPO WA BANKI na riba za mabanki yetu nahofia naomba ukae na mshauri wako mlipitie hilo kwanza....
 
Biashara unataka kufungua maeneo gani uwenda ukapata mawazo mazuri ya biashara katika ilo eneo,umkopo wa bank kwa kukushauri boara uanze na mtaji mdogo baadae ndio utajua uchukue mkopo,maana mkopo kwa biashara mpia ni risk sana jaribu kuanza kwanza japo ujue kama mkopo utaweza rudisha
 
Back
Top Bottom