Wazo la Biashara ya TRICYCLE MOTOR (BAJAJI)

lossoJR

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
2,711
Reaction score
2,384
habari wakuu.
najua wengi wenu mpo katika changamoto za kutafakari ni mradi gani wa kuwekeza pesa yako ili iwe katika rotation.
Ila mawazo mengi hupuuzwa labda kwakusosa usimamizi au undani wa Biashara husika(information).
Ila mimi Leo natoa wazo juu ya bishara ya BAJAJI(almaarufu).
hii Biashara inalipa sana na imekuwa moja ya kitega uchumi endapo yafuatayo yatazingatiwa;-
1. Uhitaji wa kutosha(wateja)
2.Service kuzingatiwa kila wiki.
3.Dereva makini.
4.Usimamizi.

Mimi nitaongelea kwa Mbeya ambapo nimekuwa na uzoefu na kusimamia miradi mingi ya watu hasa ya usafiri. Gari za abilia na pia bajaji, hapa BAJAJI zinahudumia sehemu kubwa yenye Barabara ya Lami, hivyo ni nadra sana BAJAJI kukuta imechoka kutokana na ubovu wa barabara japo Huduma kubwa ni kutoa watu katikati ya mji na kupeleka nje ya Mji.
japo mambo ni Mengi ya Kufahamu juu ya hii Biashara,nitayajibu kwa maswali.
Ila Nina kila SABABU kuwakaribisha ndugu zangu wa mikoa yote kuwekeza juu ya Biashara hii hapa Jijini Mbeya,hata wale waliozifanya BAJAJI zao katika Huduma za usafirishaji wa kidigital nashauri
wahamie na upande huu,kwani huko watachelewa kurudisha pesa zao..
Usihofu kuhusu USIMAMIZI kwani ni moja pia ya sababu ya kuanzisha mjadala huu.haya huwa makubaliano yangu pamoja na mmiliki wa chombo.
Karibuni sana tena sana kwa fursa na maswali.
 
Hayo makubaliano ni yapi mkuu
Jinsi ya uendeshaji wa Biashara yake boss.
Kuna aina mbili ya uendeshaji ambayo imezoeleka,Mosi. Boss hutaka ufanye kivyovyote ndani ya mwaka wa kwanza amerudisha pesa yake ya manunuzi na mwaka unaofuata anataka uwe wa faida.then anakuachia bajaji jumla.(yaani ndani ya miaka miwili awe amerudisha pesa na faida yake)
Lakini pili ni uendeshaji huu tuliouzoea wa 25,000 per day(siku sita za kazi) maana jumapili ni service.
 
Hayo makubaliano ni yapi mkuu
Pia kumbuka malengo ya 25,000 ni kwa bajaji mpya tu.
Bajaji ikiwa katika hali ya kawaida huwa 20,000 ikiwa hoi zaidi huzidi kupungua.
 
Ili uweze kurealise faida ya Bajaj/Boda boda yakupasa uzimiliki zaidi ya 3!.
Na kubwa kuliko yote "kama boss usikubali kutoa chombo yako kwa hesabu ya siku, itoe kwa mkataba(miezi 18-20)".
 
Ili uweze kurealise faida ya Bajaj/Boda boda yakupasa uzimiliki zaidi ya 3!.
Na kubwa kuliko yote "kama boss usikubali kutoa chombo yako kwa hesabu ya siku, itoe kwa mkataba(miezi 18-20)".
Naam,hili pia huwa linafanywa mkuu,kama nilivyoelezea ni makubaliano ya boss na msimamizi(Mimi) yeye nikusubiri hesabu tu.
Japo hata weekly or monthly collection Si haba
 
Good Deal
 
mkuu nifumbue macho kidogo,
1.Bei ya bajaji mpya kwa sasa ni kiasi gani?
2.Kama mkataba wa miaka miwili ili uachiwe bajaji,then daily utakuwa unapeleka kiasi gani kwa bosi?
3.Je bajaji itakuwa inaishi kwako ama baada ya muda wa kazi inarudi kwa boss?
4.Je bajaji ikipotea ama kupata ajali kwa uzembe wa dereva nani atawajibika?
 
akijibu unitag
 
Naam,hili pia huwa linafanywa mkuu,kama nilivyoelezea ni makubaliano ya boss na msimamizi(Mimi) yeye nikusubiri hesabu tu.
Japo hata weekly or monthly collection Si haba
Mimi boss ntahitaji kwa siku niletewe 25,000.
Wewe kama msimamizi unafaidika vipi!?..
 
1. 7.2M - 7.3M eneo/mkoa
2. 15-25 eneo/mkoa
3.Chombo ya dereva, Mali ya Boss
4. Dereva (mkataba)/ Boss (hesabu)
 
3
4

Sijazielewa vyema ndugu
3.Je bajaji itakuwa inaishi kwako ama baada ya muda wa kazi inarudi kwa boss?
Mkataba wowote ule au Hesabu yeyote ile chombo (Bajaj) itakuwa chako dereva kitalala utakapotaka wewe dereva mpaka mtakapo malizana/vunja makubaliano yenu lakini bado Bajaj itahesabika ni mali ya Boss (Leasing).
4.Je bajaji ikipotea ama kupata ajali kwa uzembe wa dereva nani atawajibika?.
Ikipotea/ ajari kama ni mkataba matengenezo na hasara ni juu yako Dereva but Ikipotea/ajari na ni hesabu basi Boss utahangaika kuitafuta zaid ya dereva.
 
OK swali nzuri boss.
1.bei bajaji kwa Mbeya ni mill 7.2(discounted).
Kwa dar es salaam kwa sasa sijajua yaweza kuwa chini(hii ni aina ya TVS).

2.haitakiwi kuzidi 30 per day kama ni kwa mkataba wa kuachiana bajaji. Na service ni juu yangu, ila kwa ule utaratibu wa 25,000 per day service ni juu yako.

3.hapa ni maamuzi yako mkuu,japo
Wengi hulala nazo. Kwasababu sometime kunakazi za night. Au kuamka mapema kuchukua abiria wa kusafiri mikoani,so ikiwa kwako ni usumbufu.
Pia imagine upo DAR na umenikabidhi bajaji mbeya,of cause lazima itakuwa chini yangu.

4.muwajibikaji ni Mimi msimamizi kwasababu ndio jukumu langu kuhakiki chombo IPO safi,chombo INA service pia imelipiwa vibali vyote kwa Wakati.
 
Mimi boss ntahitaji kwa siku niletewe 25,000.
Wewe kama msimamizi unafaidika vipi!?..
Mimi pia najilipa boss japo waweza kuta ndani ya muda kiasi, maana muda mwingi pesa ya boss ndio inaumiza akili itimie,ndio maana wengi hununu NEW ili kupata at list 25 kila siku kwa siku sita
 
Mimi pia najilipa boss japo waweza kuta ndani ya muda kiasi, maana muda mwingi pesa ya boss ndio inaumiza akili itimie,ndio maana wengi hununu NEW ili kupata at list 25 kila siku kwa siku sita
Unajilipaje?.. Kiasi gani!?.. sawa unaweza pewa simamia lakini malipo yako una uhakika yatapatikana?..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…