Wazo la biashara ya utalii

Wazo la biashara ya utalii

kiraremapojoni

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2018
Posts
391
Reaction score
512
Habari wana kijiwe? kutokana na ugumu wa maisha kwa awamu hii yatano na nina vijiakiba vyangu nimeonelea kuanzisha biashara angalau nipambanae na hali yangu. Inafahamika kama biashara zimekuwa ngumu sana kiasi ambacho watu tumekuwa tukikatishana tamaa ya kufanya biashara kwani tunaamini kama hazilipi kama ilivyokuwa zamani

Wazo langu hasa ni kufungua kampuni ambayo itakuwa inatoa huduma ya kitalii mkoani, kwa maana ya kupokea wageni na kuwatembeza kama ambavyo ratiba zao wamepanga katika tariba zao na ikiwa kuna uwezekano pia kuwaandalia malazi na chai ya asubuhi .

Na mkoa hasa ambao ninafikiria kufanya hii biashara ni Tanga nikijiaminisha kama mapango ya Amboni, Tongoni Ruins, Magoroto, Pangami, Lushoto na sehemu nyengine ambazo tutakuwa tunaziona kaam zitafaa kwa ajili ya kutembelewa na wageni


Kwa wale ambao wana uelewa kidogo naomba mwongozo wa wapi pa kuanzia ili niweze kufanikisha azma yangu

Kwa pamoja Tunaweza
 
Nenda arusha chukua course ya utour guide kwa mwez.mmoja. tafuta lesenj kubwa omba ajira kwenye kampunj kubwa. Fanya kazi kama mwaka mmoja ukiwa kama guide na kutengeneza connection ya jisni ya kupata wageni na mtaji. Connection utaipata pale unapokuwa unapenda chukua mawasilano na watalii. Baada ya mwaka uwe na kiasi cha usd kama 3000, fungua website ya utalii sajri kampuni na lipia usd 2000 kuisajiri web yako. Fungua ofisi ndogo. Wafanye wale wazungu waliokuwa waliokuja kwako na ukawa guide wao kama mawakala wako wa kutafuta wageni.
Mfano yeye anaweza pata mgeni labda sweden akamwambia gharama ya kila kitu per day ni usd5000. Ila yake akachukua 2500.ile inayobaki ndo wewe unahangaika nayo kwa usafiri,chumba,chakula na entrance fee per day. Hapo ticket ya ndege toka kwao haikuhusu.
Ni biashara nzuri na wengi wanaomiliki hizi kampuni wanajidondosha wenyewe. Usiniulize maswali mengi
 
wenye kujua z~idi Mambo ya utalii ni wenyeji na waliokulia na kuishi kilimanjaro, Tanga na Arusha alllo ni kelele sana.

zanzibar pia waliofanikiwa kwenye utalii stori zao ni Kama za mabaharia ama wachimba madini Yaani one day Yes..

katika hii Biashara huitaji kusoma sijui tourguide ama kusajili website wala kulipia tanapa na kinapa ama kuwa na tala.....ni ujanja zaidi Ila ukitaka kuifanya inavotakikana ni Biashara ngumu na inahitaji mtaji mkubwa na sheria ngumu


kwa vijana wa mjin aka day walker (day waka ama waka waka) kwa watu wa mo town wanaelewa hii maneno ni kelele dingi lai. unahitaji tu watalii hayo mengine yote hayakuhusu kisha unaenda kumdalalia huyo mtalii kwenye makampuni lakini kwa brokers wakongwe Wenye koneksheni kila kitu ana maliza mwenyewe na kukunja mpunga wote.......ana irganise kila kitu na yeye anakuwa incharge.....hii Biashara elimu haina umuhimu sana Kama uzoefu.

utalii ni neno mtambuka Yaani kuna nyanja nyingi ama namna nyingi za kufanya utalii mtu akikwambia anajua kila kitu Sio kweli binafsi nimefanya Hiyo Mambo miaka kibao na kuishi na wadau tour directors, conservators, operators, hosts lakini huwezi jua kila kitu vingine ni Kama story tu kusikia ama myths. SELL or GET SOLID

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom