Wazo la kijinga nililolipata leo.

Wazo la kijinga nililolipata leo.

Askarimtu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
277
Reaction score
185
Paap...!

Nimeamka asubuhi nikawaza jinsi tu waafrika tunavyojidharau. Nikasema kwa nini tusiwakomeshe wazungu siku moja?? Tuchukue madini yetu, tutumie kama pesa...yaani nipe dhahabu nikurudishie chenchi almasi tatu. Toa Tanzanite, nikurudishie rubi 100. Kwanza tunaishije masikini, si tujianzishie tu masoko ya barter trade? Una unga kilo 100 lakini huna mboga, mjinga wewe!!! Njoo nikupe kilo 20 za nyama ya mbuzi, unipe kilo 50 za unga. Biashara ni makubaliano. Nikiwa mkubwa nitaanzisha barter trade upya, no...nikimaliza shule....no...nikirudi Tanzania.Website zitakuwa nyingi tu, hatuwezi kulala na njaa bhana kizembe wakati sote ni ndugu!

Lakini baadae nikaona ni wazo la kijinga.

Ila nikafikiria, hivi hawa watu waliotuibia historia yetu na kufanya ya kwao nitawapikuje?? Kisasi sipendi, ila nataka watoto wangu wafahamu kuwa vitu vikubwa vyote vilitoka Afrika, Afrika itaendelea kutajirisha na kulisha dunia nzima mpaka nchi ya sasa itakapopita. Nataka nibadilishe zile movies zote zenye historia yetu na kufanya ziigizwe upya na waafrika. Nani atanipa bajeti ya bilion 1 za kitanzania nikamilishe ndoto yangu?? Looh...! Ujinga sometimes ni kichangamsha kichwa tu, kwani hukuwahi kusikia kuwa akili nyingi huondoa maarifa??

Jioni imefika, nipe wewe wazo lako la kijinga ulilolifikiria ulipoamka leo ukiachana na wazo la kunywa supu ya kongoro!!!
 
Hahaaa! Mzungu aliweka pesa ndo itawale manunuzi ya kila kitu, hata ukipewa dhahabu chumba kizima kama huna pa kuiuza ni useless
 
Unaonaje tukenda kuwatawala Wazungu kama walivyofanya wao kwetu siku zile? Hapana, sio wazo zuri. Sasa zamu yao; tuwaibie teknolonia yao ili sisi tutawale dunia sasa. Unaonaje?
 
Huna habari kwani, kuwa tumeanza kufanya feedback mechanism?? Assume tu black-american wakisepa ile nchi, nani atabaki mwanamziki? Nani atabaki mcheza boxer?? Tunawaachia Hazard, tunachukua ng'olo kante na kaka zake! Halafu tunawaambia haya tunabaki na madini yetu, vigae, madini yanayotengenezea vyuma vya ndege, na malighafi zote muhimu....hatutaki kuwauzia watu nje ya Africa! Kwa njia hii tutawatawala...sema tu watu wanaogopa kupigwa bomu la nyuklia na kusingiziwa kesi.
 
Naona kwa mbaaali hukupoteza mda darasani hasa kwenye somo la lugha.

Sent using Jamii Forums mobile app
masomo niliyokuwa nafeli ni lugha...hasa kiswahili...mwalimu alikuwa ananichanganya eti ''sina budi kufika shuleni mapema''. Sasa nikimuuliza kwani hiyo budi ni nini?? Mwalimu anasema ndivyo ilivyo hiyo. Kwanini tusitumie nina budi?? Akasema hiyo sio kiswahili fasaha. Kwanzia hapo sikuelewaga tena lugha.
 
Unaonaje tukenda kuwatawala Wazungu kama walivyofanya wao kwetu siku zile? Hapana, sio wazo zuri. Sasa zamu yao; tuwaibie teknolonia yao ili sisi tutawale dunia sasa. Unaonaje?

The DODOMA CONFERENCE for scramble and partition of Europe.
African colonizers went to colonise Europe seeking cheap labour. 😂
 
Hilo sio wazo la kijinga kwani hata Colonel Gaddafi alitaka kufanya hivyo na kutengeneza sarafu za dhahabu kama currency ya Africa baada ya kuungana na alidhamiria aanzishe Kweli huko Libya
Hapo ndio wazungu wakaona Ahaaaa kwa hiyo $ iporomoke
Ndio ukawa mwanzo wa figisu
Yaani na wewe ungekuwa Rais ukaja na wazo hili mwisho wako ungekuwa huo [emoji55]
Sio wazo baya

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Leo nimewaza namna ninavyoweza kutumia pesa ikiwa nitaokota sh.mil.50
 
mawazo ya vijana...cha kwanza gari, cha pili nyumba, cha tatu biashara...nne kustarehe. Sadaka jero ...so sad!!!
 
Hilo sio wazo la kijinga kwani hata Colonel Gaddafi alitaka kufanya hivyo na kutengeneza sarafu za dhahabu kama currency ya Africa baada ya kuungana na alidhamiria aanzishe Kweli huko Libya
Hapo ndio wazungu wakaona Ahaaaa kwa hiyo $ iporomoke
Ndio ukawa mwanzo wa figisu
Yaani na wewe ungekuwa Rais ukaja na wazo hili mwisho wako ungekuwa huo [emoji55]
Sio wazo baya

Sent from my iPhone using Tapatalk
Ndio maana democracy watu wanasemaga ni mfumo wa shetani. One day we'll rise again.
 
Back
Top Bottom