Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Ujamaa shop
Kama una mtaji mdogo, unaweza kufanya biashara hii huku ukijitengenezea 'brand' 'ujamaa shop'
Kama una mtaji mdogo, unaweza kufanya biashara hii huku ukijitengenezea 'brand' 'ujamaa shop'
- Tembelea vijiji 2 au zaidi kutokana na nafasi uliyonayo
- Anzisha maduka madogo madogo yenye muonekano wa gende; yatakayokuwa yanauza vitu vidogo vidogo kama vile vile; kiberiti, sukari ya kufunga, vitunguu, majani ya chai, viazi mviringo, dagaa, tangawizi, iliki n.k
- Tumia hayo maduka kukusanya bidhaa kijijini na kuleta mjini, mfano kuku, mayai, mbuzi, sungura n.k
- Unaweza kuanza na viduka 5, vitakavyotofautiana kwa umbali usiopungua kilomita 2 au 3.
- Tafuta kijana wa kijijini hapo, ndio umuajiri kwenye hilo duka. Kwa sababu wewe ushakuwa mwekezaji wa eneo hilo, na unatoa ajira kwa vijana/wazawa.
- Ongeza vijiduka vingi vingi, kutokana na uwezo wako, kwa vijiji mbalimbali.
- Tathmini hali ya soko, na tumia njia mbalimbali ili kuongeza mauzo.
- Fanya ukaguzi kwa kutengeneza mfumo, ili vijana wasikuibie sana.