Wazo la kutengeneza kikundi cha vijana wajasiliamali

Sikukatishi tamaa ila ukifanikiwa kuwaweka kikundi na mkafanya jambo hususani la kiuchumi mimi nitajitoa JF - Labda lingekuwa WAZO LA MAANDAMANO YA KISIASA, Ungefanikiwa kwa 100%
Kujitoa kwako JF hakuna hasara wala faida ni sawa na nanihiiii alivyohamia nanihiiii.
 
Sikukatishi tamaa ila ukifanikiwa kuwaweka kikundi na mkafanya jambo hususani la kiuchumi mimi nitajitoa JF - Labda lingekuwa WAZO LA MAANDAMANO YA KISIASA, Ungefanikiwa kwa 100%
ok sawa nimekuelewa
 
ONYO : Kuweni makini sana na kazi za vikundi. Utapeli upo wa aina nyingi sana .
naamini utapeli upo sana hapa mjini, lakini naomba nikutoe wasiwasi,
Hakuna kitu tutakachokifanya bila maandishi kupitia serikali na kujua unapoishi yani permanent settlement na tujue familia yake ndipo tumpe dhamana yeyote, katika hili letu hakuna mtu atakayeweza kupewa dhamana yoyote pasipokua na vithibitisho kama hivyo
 

Siku zote kudraft ndio shida, nakupa hongera sana maana umetufumbua macho tulio wengi
Mchango wangu ni kama ifuatavyo
Kwakuwa umeonyesha nia ya kufanya biashara ya chakula ni vema kujua wateja wako (soko/demand) ili kuifanya biashara iweze kuwa stable na kukuwa
Kwa biashara ya chakula ni vema kulenga wateja wa kipato cha kati
Hapa nazungumzia watumishi wa serikal na sector binafsi na wafanya biashara pia.
Wateja wenye vipato vyakat wanauzur ufuatao
Wao daima upenda mzingira masafi na chakula chenye ubora na atalipa fedha inayo fanan na mazingira hayo na utamfanya hata kesho arudi tena ( wanapenda ustaarabu) hi itapelekea kuongeza ufanis na faida pia maana kila jambo zur utakalo ongeza litakuwa na thaman ya soko (money value)
Ila biashara ya chakula ambayo inalenga wateja wa kipato cha chini ( sahan 1500) ni ngum sana na haina maisha marefu maana wateja wao ujali ujazo na sio ubora
Mara zote wao ni watu wakuamaama kutafuta ujazo na wateja wako wengi watakuwa makonda, mafundi wadogo wadogo watengeneza bikipik na baskel na madereva wa bodaboda yupo radhi atoke ubungo akale tabata kisa ujazo wa chakula bila kujar katumia mafuta ya kias gan.
 
ulichokizungumza hapa ni cha msingi sana na nilipenda nipate watu wenye mawazo kama haya,sasa ili tusiibue mjadala mwingine kwakua mimi nimetoa proposal tu na tunatarajia kukutana naomba siku hiyo iwe ndiyo ya kuchambua mambo yote haya yaliyo ndani ya hii biashara tunayotaka kuanza ili kila mmoja aelewe vzr
 

Mkuu nipo shule nje ya tanzania
Mchango wowote wa mawazo nitautoa nikipewa mada
 
Wazo zuri ila mm napendekeza tujikusanye tujenge mabanda ya kuku na ng'ombe wa maziwa kisasa eneo ninalo ekari 5 madale ni pm kwa ufafanuzi zaidi
 
Wazo zuri ila mm napendekeza tujikusanye tujenge mabanda ya kuku na ng'ombe wa maziwa kisasa eneo ninalo ekari 5 madale ni pm kwa ufafanuzi zaidi
siku tukikutana naomba hili wazo uliweke mezani tuliongelee ni zuri sana ukizingatia tuna nyenzo tayari au hata kikundi chetu tutakapokianzisha whatsap naomba uweke na hili ili watu waseme wao wenyewe
 
wazo zuri ila kwa uwo mradi unaitaji mtaji mrefu na kwa hali ya sasaiv ilivo ni ngumu
mtaji hatuhitaji kuwa na milioni dadaangu, kinachotakiwa ni uthubutu wa watu kufanya kazi, hata mbuyu ulianza kama mchicha hatuwezi kukata tamaa kwa mtaji mdogo, huohuo tutakaopata tutaona biashara yoyote itakayoendana na mtaji wetu tusiumize watu bure
 
ni kweli ila mimi nilimaanisha kwa ilo wazo la ng'ombe kuku nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…