Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu angeniambia niwapi nielekeze lawama zangu, moja kwa moja ningeelekeza kwa serikali kwani hao ndiyo wanaweza kukabiliana hata kuondoa tatizo hili moja kwa moja na kwa haraka. Mimi nilipokuwa nasikia Kitu kinachoitwa Ustawi wa jamii, nilidhani ni watu ambao wakati wote huangalia na kusimamia jamii ya Kitanzania nakujua matatizo yao na kuyachukulia hatua, inavyoelekea hilo sio jukumu lao!! Niliwahi kufikiria kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ndiyo ingebeba jukumu hili ambalo sidhani kuwa ni kubwa la kuwashinda, chakusikitisha ni kwamba sijawahi kusikia mpango wowote wa maana unaoonyesha kuwa serikali imechoshwa na tatizo hili la watoto wa mitaani, jukumu hili toka zamani linaelekea kuachiwa Taasisi za dini ambazo nyingi kwa sasa hazina uwezo kutokana na kujitoa kwa wafadhili wa Kizungu ambao waliweza miaka hiyo kulibeba kwa kiasi fulani. Tatizo hili la watoto wa mitaani kwa kiasi kikubwa limeota sugu sana katika miji mikuu hasa mijini. Tatizo hili haliwezi kwisha kutokana na ubinafsi na ukosefu wa Upendo kutoka kwa viongozi wetu pia jamii kwa ujumla kuona kuwa ni kitu cha kawaida kuona mtoto akitangatanga bila kuwa na usimamizi au walezi wa uhakika. Hii ni hatari sana kwani pamoja na kuwa hatima ya watoto hawa itakuwa mbaya lakini haya ndiyo mambo yanayochangia kuongezeka kwa uhalifu na mambo yanayoendana na hayo.Wakati umefika Serikali yetu kutafuta namna ya kukabiliana na tatizo hili ili ikiwezekana liondoke kabisa aidha manispaa pamoja na Halmashauri na jamii kwa ujumla iweke mikakati madhubuti ya namna ya kukabiliana na tatizo hili, kinachokosekana hapa ni ubunifu na kutokuwa na viongozi ambao wanaliona tatizo hili la watoto wa mitaani kama changamoto, sitaki kuamini kuwa jiji kama hili la Dar linaweza kushidwa kuamua kujenda vituo maalum vya watoto hawa na kuhakikisha kuwa kila atakayekutwa anazurura mtaani hupelekwa kwenye vituo hivyo na kuhakikisha wanapewa huduma pamoja na elimu ili watoto hawa baadae wawe manufaa kwa taifa badala ya kuwa balaa kama wataachiwa kama ilivyo sasa. Haya ni mambo yanayowezekana jamani!!!!