Wazo langu: Huduma za serikali na mashina yake zianzie 7:00am hadi 3:00pm

Alpha M

Senior Member
Joined
Nov 8, 2016
Posts
165
Reaction score
156
MABADILIKO YA RATIBA UTOAJI WA HUDUMA ZA SERIKALI NA MASHINA YAKE KUANZIA 7:00AM HADI 3:00PM

Binafsi ninaamini anayeamka mapema zaidi ya mwenzake anayo nafasi kubwa ya kufanikiwa zaidi ya mwenzake (ikiwa wapo ngazi moja na wanafanya kazi masaa yanayolingana). Pia kwa wastani nchi nyingi zilizoendelea watu huamka mapema (pamoja na masaa mengi ya kazi) zaidi ukilinganisha na zile ambazo hajijaendelea. (Accrording to UNESCO)

Kila nchi inao mtizamo wake wa kazi pia utendaji wa kazi husika. Ratiba ya shughuli za kila siku hutofautiana kwa jamii moja na nyingine. Wafanya biashara wengi waliofanikiwa huamka mapema sana kabla hata ya 5:30AM na kufanya shughuli binafsi, baadae hao hao utawakuta ofisi za serikali kabla ya saa 8:00AM wanasubili huduma wakilalamika uchelewaji wa maofisa vitengo husika.

Maoni yako mwanajamvi wewe unamtizamo gani, je matokeo yatakua chanya au hasi kwa ujumla kwenye uzalishaji na utendaji wa wananchi na nchi kwa ujumla?
 
upo sawa , hata mie naunga mkono hoja hiyo ,mabadiliko yatakuwepo tena makubwa tu na kuwafanya watu kuanza kuona thamani ya muda wao
 
Hiyo ni kweli.hivi niulize swali.nani alijua kama uingereza ambayo miaka ya 1800 ilikuwa world super power na sasa ni kioja mpaka anaomba kujitoa ktk EU.hataki ushindani tena?Hivyo hatuwezi kuwashangaa wakenya ambao siku zote walitufanya shamba la bibi leo hii wanaona tunawapumulia kisogoni wanaanza kuweka threts ktk business.wawe wapole tu bidhaa iko poa tu.tupige biashara heko tz.heko mr presidaa kanyaga twende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…