Mpaka sasa nimebahatka kua na jumla ya Tsh milion 3, toka zamani nina wazo la kuanzisha saloon ya kiume ambayo ni ya kisasa kabisa na mtaa ninao kaa mpaka sasa ipo saloon moja tu ambayo sio ya kiwango sana mimi nimeona chance na kuweka hiyo saloon yangu ambayo itakua ni ya kisasa kuliko hiyo iliyopo mtaani kwetu vipi wadau niko vizuri au ntakua naleta bifu na huyo ambae tayari anayo ya kwake.
Je pia hili ni wazo zuri au ntakua nimeingia choo cha kike harusini?