Wazoefu wa biashara ya parachichi nina swali

Wazoefu wa biashara ya parachichi nina swali

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari wakuu,

Kuna mahali nataka kwenda kununua tani kadhaa za parachichi ila sasa huko kijijini wauzaji wanauza kwa kipimo cha ndoo (debe).

Naomba kujua kwa wenye uzoefu, ndoo moja ya lita 20 ikijaa parachichi inaweza kuwa na wastani wa uzito wa kilo ngapi?

Natanguliza shukrani.
 
Acha mbwembwe ,yaani uwe na project ya kununua tani kadhaa halafu ushindwe kwenda shamba kujaza ndoo na kupima uzito unaumwa malaria kali wewe.
Anatushirikisha jamiiforum kwanza, halafu kesho ataanza kuaga majirani ndugu jamaa na marafiki, halafu ajipange na safari wiki ijayo ndio akakate tiketi aende huko kijijini kununua mzigo.
 
Acha mbwembwe ,yaani uwe na project ya kununua tani kadhaa halafu ushindwe kwenda shamba kujaza ndoo na kupima uzito unaumwa malaria kali wewe.
Ni mbali mkuu. Siwezi kufunga safari yote hiyo bila kuwa na hesabu kamili nione kama biashara italipa au la. Lengo langu ni kuwa na estimation ya bei ya tani maana nimepewa bei ya ndoo.
 
Ni mbali mkuu. Siwezi kufunga safari yote hiyo bila kuwa na hesabu kamili nione kama biashara italipa au la. Lengo langu ni kuwa na estimation ya bei ya tani maana nimepewa bei ya ndoo
Mbali nje ya nchi, au?! Mathalani upo Dar es salaam, je Soko la Stereo Temeke nako mbali?! Na popote ulipo, kuna masoko mangapi sawa na Soko la Stereo, Temeke?! Kama unaweza kununua tani kadhaa, utashindwaje kwenda Stereo kununua ndoo moja ya maparachichi?! Au hata ukitoa Sh 10K kwa muuza maparachichi ukamwambia shida yako ni kufahamu tu ndoo 1 ya parachichi ni kilo ngapi, unadhani ataiacha hiyo 10K wakati mizani zipo hapo hapo jirani yake?!
 
Ni mbali mkuu. Siwezi kufunga safari yote hiyo bila kuwa na hesabu kamili nione kama biashara italipa au la. Lengo langu ni kuwa na estimation ya bei ya tani maana nimepewa bei ya ndoo
Haya kaa hapo hapo kama umepigiwa misumari.
 
Wanyakyusa mupoooo....!!!!!👋.
 
Ni mbali mkuu. Siwezi kufunga safari yote hiyo bila kuwa na hesabu kamili nione kama biashara italipa au la. Lengo langu ni kuwa na estimation ya bei ya tani maana nimepewa bei ya ndoo.
wewe si ukanunue hata sokoni pale manzese? acha kutuchosha bhana
 
Mpaka hapo kdg mmemchangamsha akili yake maake alifkiri parachichi mpk ya kule tu ndio utakupa majibu bay the way iyo ni tenda uchwala ingekuwa ni ya uhakika saiv ingekuwa imeshakata kona ya makambako...huwezi amua mpk uguse sio [emoji2957]
 
Nenda sokoni mabibo nunua parachichi ma wili matatu piga stori mbili tatu na wafanyabiashara wa parachichi waulize maswali ya msingi kuhusu hiyo biashara changamoto zake utaondoka hapo umefahamu kila kitu. Kilala kheri.
 
Back
Top Bottom