Wazoefu wa ferry kuhusiana na biashara ya samaki naomba mnipe wazo kabla sijaumia..

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,471
Habari za majukumu wakuu...
Nimekua na mawazo sana ya kutaka kufanya hiyo shughuli ya uuzaji wa samaki lakini sio mimi binafsi ni kumpa mtu mwengine.

Sasa kinachomifanya hadi leo sijapata ufumbuzi ni kwamba,.. Sijajua faida, hasara na malipo kwa mtu ambae nataka nifanye nae hiyo biashara.

Naamini hapa ni sehemu imara na penye vichwa na wingi wa kila idara. Hapa naamini hawakosi madalali wa ferry pia wataalam waliowahi kufanya huo mchakato.

Nisiwapotezee mda sana, ishu ni kwamba, nataka niingie na mtaji wa milioni 3 kwanza niangalie mwenendo na halisi ya pale. Je naweza kufanikisha zoezi kwa mtaji huo?
 
Wazo zuri ndugu kwa pesa ya mtaji ulio nao unaweza Fanya hyo biashara
Ila naomba ntoe mchango wangu wa mawazo kidogo mana sina uzoefu mkubwa wa biashara ya samaki isipokuwa uzoefu wangu upo kwenye biashara ya pweza
Pale ferry huwa kuna madalali ambao kazi yao ni kuuza samaki kwa njia ya mnada na kwa samaki wadogo huwa wanauza kwa kwenye kikapu na kunadisha kwa wanunuzi
Kwa samaki wakubwa hua pia wanawanadisha pia ila samaki wadogo ndo huwa wanawateja wengi na pia huwa wanafaida kubwa kwa maelezo kutoka kwa wauzaji
Lakini pia unapaswa kuwa makini na dalali ambaye unataka kufanya nae hyo biashara
Kuhusu malipo ya dalali sina hakika na hili ila huwa wanalipwa kwa mapatano but sina uhakika na hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…