Wazungu\Foregners wanatengeneza sana pesa hapa nchini kwa ujinga wetu

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Nchi hii foregners hawa wana make sana pesa asikuambie mtu, usiwachukulie poa sana hawa jamaa.

Mfano kwa Arusha nimekutana na Foreigners wana make pesa kwenye vitu ambavyo tungepwaswa sisi kufanya ila ndio kama hivyo.

Kuna Foreigners anatengeneza Hand Made Soap za Kuogea,yaani ukiona anavyo zitengeneza utaamini kwabisa sisi tuna matatizo, anatengeneza Guest Soap na ana oda za Camp na Mahoteli za kitalii, ni full handa made na hata Packahing yenyewe ni matata sana. Nikakumbuka training za SIDO za watu kuzalisha sabuni za maji yaani creativities hakuna.

Mikate, hapa ndipo nilichoka kuna Dada ni wa kizungu ana oka mikate, sio hii tunayo uziana mitaani hapana mikate ya ukweli na ghari sana, mkate unatembea 10,000\ na ana wateja wake na daily anazalisha mikate 100 hadi 150 tu na inaisha yote, niliwahi jitutumua siku moja nikakununua huo mkate sema alinifanyia 5000 kwa sababu nilikuwa na mdai pesa aisee ilinifanya niache kabisa kula hii mikate yetu ya mtaani, tunauziana sponji na wala sio mikate mara 100 ninywe chai kavu.

Fanicha, nilikutana na mzungu pia anatengenezea nyumbani kwake fanicha na anazalisha kwa ajili ya wazungu wenzake na pia hizi hotel, mbao ni hizi hizi misitu yetu, cha ajabu sisi tunakomaa na fanicha za Mabox kutoka China, aisee kuna sehemu hatuko sawa. Meza mmoja unaweza itumia miaka 50 na ikawa iko sawa but tunakomaa na fanicha za mabox kutoka China sijui shida ni nini.

Hoteli za Katavi zile za utalii, Mboga na matunda zinatoka Arusha, hebu fikiria mboga zinatolewa Arusha kupelekwa Katavi National Park kwa ajili ya Wageni, Katavi sijawahi fika ila najua kuna raia.na wanalima, sasa je wanalima nini hasa?

Home made Jam, kuna mwingine pia huyo nar anatengeneza Home made Jam za ukweli na kuuzia wenzake.

Hao wote wanatengenezea nyumbani hizo Products zao na ni za viwango hasa.

Wako wengi sana wengine spice kuna anaye zalisha uyoga anauzia wenzake, kuna anayetengenezea nyumbani chakula cha mbwa anawauzia wezake, lisit ni ndefu sana ila kwa kifupi tuna shida mahali.
 
Hayo mahoteli ya katavi yanayoimport mboga toka Arusha mmiliki ni nani. Kumbuka, mkitaka kufanikiwa kama kikundi, ukoo, kabila. Ukitaka kununua hakikisha unanunua kwa ndugu yako, ila ukitaka kuuza muuzie yeyote
Ndio fitna za kukuza uchumi wa kikundi.
 
Issue sio kama wabongo hatuwezi ila kimbembe ni connection kumbuka hao unaowasema ni wenzao wanavyowachukulia ni tofauti na sisi wazawa.

Kama unabisha nenda kaombe tenda kwenye hitel yoyote ile wewe na mwarabu tu wa bongo msupply kitu uone mtavyochukuliwa nyie wawili.
 
Dunia iko chained, kwa namna fulani, gezea tengeneza uone kama utauza,
Mfano :, DP World, ni kampuni ipo chained kwa kiasi kikubwa inajipakizia mizigo toka nchi fulani inajipelekea nchi fulani, infact inajitahidi kuhodhi biashara ya usafirishaji in networking program, usipoelewa haya yanayoendelea duniani utachelewa kweli na ushuhudie ukidorora.
 
kama unaona ni kazi rahisi jaribu kutafuta tenda hata kwa Mtanzania mwenzako kusambaza sabuni uone kama utapata.. haya maisha yapo channelled sana mkuu, ningekupa kisa kimoja cha kampuni mbili kubwa hapa nchini na watu wanaofanya nao kazi ungechoka, basi tu kwa sababu za kiusalama siku nyingine. ila makampuni mengi ya kigeni yana vikampuni vidogo vidogo vinavyonaya kazi nao ambavyo ukifuatilia ni kutoka nchi asili ya hiyo kampuni kubwa, hii ni kuhakikisha kuwa kila hela inayozalishwa na kutumiwa na kampuni kubwa inarudushwa kwao in indirect waya
 
Hayo mahoteli ya katavi yanayoimport mboga toka Arusha mmiliki ni nani?
Kumbuka ,mkitaka kufanikiwa kama kikundi,ukoo,kabila,. Ukitaka kununua hakikisha unanunua kwa ndugu yako ,ila ukitaka kuuza muuzie yeyote
Ndio fitna za kukuza uchumi wa kikundi
Kanuni ya wayahudi wawapo popote pale Duniani na ndio maana wana maendeleo sana,na kanuni hiyo hiyo ndio wame copy jamii kama singasinga na wahindi,chunguza hayo utajagundua.
 
Ndio nimejionea mengi kwa style hii hapa dar es salaam,wahindi wananunua mizigo kwa ndugu zao na mikopo wanapata huko India wanaleta kwa wenzao hapa bongo hata clearance wanafanya kwa wenzao wanapelekea mizigo Hadi Zambia na Malawi Hadi ma truck ni ya wahindi wenzao na ma warehouse ni ya Kwao hapa wanaajiri madereva tu na hiii hata wachina wameanza sasa hapa bongo mwisho wa siku tutakuja shtuka hakuna kazi mbongo anafanya
 
Mimi natengeneza sabuni ya kuogea 96.8% ni herbal lakini watu hawaniungishi wanataka vitu kutoka mbali
 
Connection ndio kila kitu. Hao wanapeana wenyewe. Ukienda wewe hupewi ng'o.

Foreigners wengi ndivyo wanavyofanya hivyo. Wanapeana wenyewe, wanakopeshana wenyewe na kupeana kazi wenyewe. Wazungu, wahindi, wachina, waarabu, wapakistan ndivyo wanavyofanya.


Kazi za chini na za hovyo ndio mnapewa wazawa 🤣🤣
 
Tatizo linaanzia kwenye kukariri nots za masomo ..

Pia tunafundishwa Ili tugombanie white collar job..
 
Asili ya kanuni hii ya kufanikiwa kama chain imeasisiwa na wayahudi ndio wazungu, waarabu, wachina, wakinga,wachaga, uitumia hata mchaga alewi kwa bar isiyo ya jamaa yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…