bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Kabisa , tunatengeneza nchi ya vijakazi na watumwaNdio nimejionea mengi kwa style hii hapa dar es salaam,wahindi wananunua mizigo kwa ndugu zao na mikopo wanapata huko India wanaleta kwa wenzao hapa bongo hata clearance wanafanya kwa wenzao wanapelekea mizigo Hadi Zambia na Malawi Hadi ma truck ni ya wahindi wenzao na ma warehouse ni ya Kwao hapa wanaajiri madereva tu na hiii hata wachina wameanza sasa hapa bongo mwisho wa siku tutakuja shtuka hakuna kazi mbongo anafanya
Na bahati nzuri nyie ndo mnapigwa sasaVijana tumeamua kujiajiri, kuna Wakurugenzi/Mameneja na Maafisa Bashiri, kazi yetu kubwa ni kutengeneza fixture ili kumpiga muhindi.
Ukiacha uwezo wetu wa kuchakarika, lakini mifumo yetu sio rafiki kabisa kwa wazawa, kule zenj,sehemu moja inaitwa PAje kuna mzungu analima pilipili! Na ye ye ndio sole supplier kwenye ma hotel yote (yanayomilikiwa na wazungu pia), we m Swahili kupata hii tender, may be uwe mtoto wa waziri.Nchi hii foregners hawa wana make sana pesa asikuambie mtu, usiwachukulie poa sana hawa jamaa.
Mfano kwa Arusha nimekutana na Foreigners wana make pesa kwenye vitu ambavyo tungepwaswa sisi kufanya ila ndio kama hivyo.
Kuna Foreigners anatengeneza Hand Made Soap za Kuogea,yaani ukiona anavyo zitengeneza utaamini kwabisa sisi tuna matatizo, anatengeneza Guest Soap na ana oda za Camp na Mahoteli za kitalii, ni full handa made na hata Packahing yenyewe ni matata sana. Nikakumbuka training za SIDO za watu kuzalisha sabuni za maji yaani creativities hakuna.
Mikate, hapa ndipo nilichoka kuna Dada ni wa kizungu ana oka mikate, sio hii tunayo uziana mitaani hapana mikate ya ukweli na ghari sana, mkate unatembea 10,000\ na ana wateja wake na daily anazalisha mikate 100 hadi 150 tu na inaisha yote, niliwahi jitutumua siku moja nikakununua huo mkate sema alinifanyia 5000 kwa sababu nilikuwa na mdai pesa aisee ilinifanya niache kabisa kula hii mikate yetu ya mtaani, tunauziana sponji na wala sio mikate mara 100 ninywe chai kavu.
Fanicha, nilikutana na mzungu pia anatengenezea nyumbani kwake fanicha na anazalisha kwa ajili ya wazungu wenzake na pia hizi hotel, mbao ni hizi hizi misitu yetu, cha ajabu sisi tunakomaa na fanicha za Mabox kutoka China, aisee kuna sehemu hatuko sawa. Meza mmoja unaweza itumia miaka 50 na ikawa iko sawa but tunakomaa na fanicha za mabox kutoka China sijui shida ni nini.
Hoteli za Katavi zile za utalii, Mboga na matunda zinatoka Arusha, hebu fikiria mboga zinatolewa Arusha kupelekwa Katavi National Park kwa ajili ya Wageni, Katavi sijawahi fika ila najua kuna raia.na wanalima, sasa je wanalima nini hasa?
Home made Jam, kuna mwingine pia huyo nar anatengeneza Home made Jam za ukweli na kuuzia wenzake.
Hao wote wanatengenezea nyumbani hizo Products zao na ni za viwango hasa.
Wako wengi sana wengine spice kuna anaye zalisha uyoga anauzia wenzake, kuna anaye tengenezra nyumbani chakula cha mbwa anawauzia wezake, lisit ni ndefu sana ila kwa kifupi tuna shida mahali.
Na Bado wanasisitiza elimu Kwa kiswahiliUkiacha uwezo wetu wa kuchakarika, lakini mifumo yetu sio rafiki kabisa kwa wazawa, kule zenj,sehemu moja inaitwa PAje kuna mzungu analima pilipili! Na ye ye ndio sole supplier kwenye ma hotel yote (yanayomilikiwa na wazungu pia), we m Swahili kupata hii tender, may be uwe mtoto wa waziri.
Kwa hotel za zenj, hutegemea mboga mboga, nysnya, na mayai kutoka bara,lakini bara haiwezi kukidhi mahitaji, mpaka inabidi waagize kutoka South Afrika,
Nilichojifunza, ukitaka kutoka na kupiga pesa, kwanza tuache kuwaza kama wajamaa, kupenda kusaidiwa, tunatakiwa tuwe aggressive(mkinga,haya, chaga wanayo hii), pili luggage ni muhimu Sana,
Nimeshuhudia wa Kenya wanachukua tender za hapa bongo ki uraisi Sana, kwanza wanajua kujieleza vzr, Hawa wenzetu weupe unafika hotelini kwake unataka kuomba tender ya kumletea mboga mboga, au kuhudumia vifaa vyake vya umeme, unapewa nafasi uongee unaanza ze zeee ze, wanakuona wa maana ukipiga ngeli ikaflooow kama maji.
Uko sahihi kabisa, watu hawafahamu tu.Issue sio kama wabongo hatuwezi ila kimbembe ni connection kumbuka hao unaowasema ni wenzao wanavyowachukulia ni tofauti na sisi wazawa.
Kama unabisha nenda kaombe tenda kwenye hitel yoyote ile wewe na mwarabu tu wa bongo msupply kitu uone mtavyochukuliwa nyie wawili.
Kweli kabisa.Connection ndio kila kitu. Hao wanapeana wenyewe. Ukienda wewe hupewi ng'o.
Foreigners wengi ndivyo wanavyofanya hivyo. Wanapeana wenyewe, wanakopeshana wenyewe na kupeana kazi wenyewe. Wazungu, wahindi, wachina, waarabu, wapakistan ndivyo wanavyofanya.
Kazi za chini na za hovyo ndio mnapewa wazawa 🤣🤣
Shule ya Atlas, kwanza kupata tenda kazi na ukipata tenda unasupply malipo wanakuzungusha. Ila alikuja mchina ana supply mkaa, yani wanamlipa kabla hata ya kuleta huo mkaa. Sisi ngizi nyeusi tunabaniana sanaIssue sio kama wabongo hatuwezi ila kimbembe ni connection kumbuka hao unaowasema ni wenzao wanavyowachukulia ni tofauti na sisi wazawa.
Kama unabisha nenda kaombe tenda kwenye hitel yoyote ile wewe na mwarabu tu wa bongo msupply kitu uone mtavyochukuliwa nyie wawili.
na kweli, mbona yeye analaumu wabongo wenzie wakati yeye pia hizo fursa hajatumia? au hazitaki.S
SHIDA IPO KWAKO KWA KUTOTUMIA HIZO FURSA.
Mnafukuza dp World mtajifunza wapi Sasa, endeleeni kukomaa na Chadema na ccm badala ya kutafuta fursaTujifunze kwao
Hao foreigners wameingiaje nchini.Nchi hii foregners hawa wana make sana pesa asikuambie mtu, usiwachukulie poa sana hawa jamaa.
Mfano kwa Arusha nimekutana na Foreigners wana make pesa kwenye vitu ambavyo tungepwaswa sisi kufanya ila ndio kama hivyo.
Kuna Foreigners anatengeneza Hand Made Soap za Kuogea,yaani ukiona anavyo zitengeneza utaamini kwabisa sisi tuna matatizo, anatengeneza Guest Soap na ana oda za Camp na Mahoteli za kitalii, ni full handa made na hata Packahing yenyewe ni matata sana. Nikakumbuka training za SIDO za watu kuzalisha sabuni za maji yaani creativities hakuna.
Mikate, hapa ndipo nilichoka kuna Dada ni wa kizungu ana oka mikate, sio hii tunayo uziana mitaani hapana mikate ya ukweli na ghari sana, mkate unatembea 10,000\ na ana wateja wake na daily anazalisha mikate 100 hadi 150 tu na inaisha yote, niliwahi jitutumua siku moja nikakununua huo mkate sema alinifanyia 5000 kwa sababu nilikuwa na mdai pesa aisee ilinifanya niache kabisa kula hii mikate yetu ya mtaani, tunauziana sponji na wala sio mikate mara 100 ninywe chai kavu.
Fanicha, nilikutana na mzungu pia anatengenezea nyumbani kwake fanicha na anazalisha kwa ajili ya wazungu wenzake na pia hizi hotel, mbao ni hizi hizi misitu yetu, cha ajabu sisi tunakomaa na fanicha za Mabox kutoka China, aisee kuna sehemu hatuko sawa. Meza mmoja unaweza itumia miaka 50 na ikawa iko sawa but tunakomaa na fanicha za mabox kutoka China sijui shida ni nini.
Hoteli za Katavi zile za utalii, Mboga na matunda zinatoka Arusha, hebu fikiria mboga zinatolewa Arusha kupelekwa Katavi National Park kwa ajili ya Wageni, Katavi sijawahi fika ila najua kuna raia.na wanalima, sasa je wanalima nini hasa?
Home made Jam, kuna mwingine pia huyo nar anatengeneza Home made Jam za ukweli na kuuzia wenzake.
Hao wote wanatengenezea nyumbani hizo Products zao na ni za viwango hasa.
Wako wengi sana wengine spice kuna anaye zalisha uyoga anauzia wenzake, kuna anaye tengenezra nyumbani chakula cha mbwa anawauzia wezake, lisit ni ndefu sana ila kwa kifupi tuna shida mahali.
Sio kweli.. Kuna Makabila hapa Tanzania usipojua lugha yao hawanunui bidhaa zako.Kitu nilichokiona kwa wabongo yani kuliko mtu amuungishe rafiki yake au ndugu ni bora akanunue kwa mtu asiyemfaham.Nilichojifunza kwa wahindi yani kununua vitu kwa muhindi mwenzake ni jambo la kawaida kabisa ila sisi wabongo tuna roho kubwa. Hata ukiangalia watu wengi waliofanikiwa hawana roho kubwa wako humble tuu ndio maana baraka zinazidi kuwashukia.