Wazungu walishangaa sana kwa ustaarabu na utamaduni uliokuwa kwa wahaya kabla ya wakoloni

Wazungu walishangaa sana kwa ustaarabu na utamaduni uliokuwa kwa wahaya kabla ya wakoloni

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Tukiweka ushabiki pembeni, na kuangalia ukweli ni kwamba wazungu walishangaa Sana aina ya utaratibu na muundo wa kiserikali waliokuwa nao wahaya kipindi wanakuja kutawala miaka ya 1800,

Ndipo maana waliamua kuwasomesha wahaya na kuwategemea katika usimamizi wa shughuli zao nyingi, ilikuwa rahisi Sana kukaa Uhayani saa nyingine hata uchagani kuliko sehem nyingine yeyote,

History yenyewe
Wenyeji wake waliitwa na wakoloni Wahaya, ingawa baada ya kupata wilaya yao, baadhi ya wenyeji wa Karagwe walikataa kuitwa Wahaya. Akifafanua chanzo cha jina hilo, Mjerumani Stuhlmann aliandika mwaka 1899 kuwa lilikuwa ni jina la maeneo ya Mukama Kishebuka na Mukama Bwahama wa Kiamutwara, hasa yale yaliyo kwenye mwambao wa ziwa.

Kila moja ya makabila haya ilikuwa inatawaliwa na Mukama , na kila Bukama iligawanywa katika gombolola zilizokuwa zinaongozwa na abami. Kila gombolola ilikuwa na vijiji kadhaa vilivyoongozwa na abakungu. Kabla ya wakoloni kuja, Mukama alikuwa absolute ruler, kwa maana kwamba, neno lake lilikuwa ni sheria na ardhi yote ilikuwa ni mali yake.Kadhalika hata watu, mifugo na misitu vyote vilikuwa ni mali zake.

Kiongozi wa secretariat yake aliyekuwa na umaarufu mkubwa alikuwa ni Omwami Francisco Xavier Rwamugira aliyejulikana kama Omukama wa mwenda. Kwa kuwa alikuwa Mziba, alisababisha watu wengine kuwachukia Waziba, kutokana na hisia kuwa Rwamugira alikuwa anapendelea watu wa Kiziba.

Mzungu wa kwanza kukanyaga Bukoba alikuwa ni Mjerumani Emin Pasha aliyewasili tarehe 31 Oktoba, 1890, ingawa miaka 30 kabla ya hapo Waingereza wawili, T.H. Speke na T.A Grant waliwahi kufika Karagwe na kukutana na Omukama Rumanyika l (Rugundu). Gavana wa kwanza wa kijerumani ni Julius von Soden 1891-1893 na wa mwisho ni Heinrich Schnee (1912-1916).

Gavana wa kwanza wa kiingereza ni Sir Horace Byatt (1916-1924) na wa mwisho ni Sir Richard Turnbull (1958-1961).
Sisi Bahaya (wakiwemo Banyambo) tunajulikana kama Western Interlacustrine Bantu. Tulihama kutoka Uganda Magharibi katika karne za 15 na 16, hasa kutoka Bunyoro na Ankole. Koo nyingi kama ule wa kwangu (abaziba/ababiito) asili yetu ni Bunyoro na chache kama abamiilo/abagabo asili yao ni Ankole.

Wajerumani walipoona mila zetu na lugha zetu zinafanana wakaamua kutuita Wahaya. Hivyo jina Wahaya linajumuisha Bahyoza, Bahendangabo, Baziba, Bahamba, Banyaihangiro, Banyambo, Bakara na Babumbiro.


Ikumbukwe hata baada ya wakoloni kuondoka wameacha wahaya ndo kabila lililoshika nyadhifa muhimu,

Nyerere aliamua kuwatumia pia katika shughuli zake baada ya mwaka 1958 wao kama bahaya kudai Uhuru wao chini ya Mukama Rutinwa, na hii slogan ilisumbua sumbua mpaka mwaka 1963 walipowasilisha tena hoja ya kuwa nchi huru,

Nyerere hakutumia nguvu alichofanya ni kuwapa uongozi serikalini waliokuwa na hoja hiyo

Britanicca
 
Kuna muhaya mmoja alikuja kuosha gari kweny petrol station yangu sasa ikawa anajitapa sana sisi wahaya mara hivi mara vile basi mzee wangu akaongea neno moja na kumwambia tokea nikae dar hii mwaka wa 60 najua sifa moja tu tena ya wahaya wanawake sio wanaume
 
Du kuna kitabu nilisoma cha familia ya wahaya, baba alikuwa dr mstaafu, alikuwa na watoto veanne wawili wakubwa mmoja aliolewa Mombasa, mmoja alikuwa nwalimu. Aliishi na watoto wake wawili wadogo pamoja na mkewe. Watoto walikuwa Kokugonza na Mjuni.
 
6. 'll 909azp





sawa 1z
IMG-20180202-WA0026.jpg
 
Du kuna kitabu nilisoma cha familia ya wahaya, baba alikuwa dr mstaafu, alikuwa na watoto veanne wawili wakubwa mmoja aliolewa Mombasa, mmoja alikuwa nwalimu. Aliishi na watoto wake wawili wadogo pamoja na mkewe. Watoto walikuwa Kokogonza na Mjuni.
Kokugonza
 
kutakuwa kuna uhusiano baina ya uzungu na papuchi, sehemu nyingi alizokaa sana mzungu jamii yake ni nyepesi sana katika kulinda bikira zao. Bukoba(haya),Moshi (chagga/pare), Masasi (makua) etc
 
kutakuwa kuna uhusiano baina ya uzungu na papuchi, sehemu nyingi alizokaa sana mzungu jamii yake ni nyepesi sana katika kulinda bikira zao. Bukoba(haya),Moshi (chagga/pare), Masasi (makua) etc
We utakuwa mkwele
 
Back
Top Bottom