BENTY
Member
- Jan 3, 2019
- 11
- 23
Waheshimiwa wana jf naomba kuelimishwa kuhusu lugha zetu wanadamu hususuni watanzania wenzangu.Hapa nchini tuna makabila zaidi ya 120 na kila kabila wana lugha yao wanayoitumia kwa mawasiliano na shughuli zingine za kila siku.Mfano mikoa ya kusini Mtwara kuna wamakonde,Ruvuma kuna wangoni, Mbeya kuna wanyakyusa na kadhalika.Makabila yote hayo kila kabila wana lugha yao tofauti kabisa na lingine.Swali langu ndugu zangu ni hili, je nani aliwafundisha kuzungumza lugha hizo kwa sababu hata mwarabu au wazungu walipokuja kwetu Afrika walikuta wenyeji wana lugha yao.Natanguliza shukrani.