Wazungu wavamia Kariakoo kusaka SAMSUNG feki

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,095

Habari toka Kariakoo zikitujuza Uvamizi wa gafla uliofanywa kwa kushirikisha Polisi na Raia wa Kizungu waliopita kwenye maduka na kuchukua simu zote za aina ya Samsung za kichina.



Baada ya kufanya mahojiano kwa njia ya mtandao na simu na baadhi ya wafanyabiashara, tulifahamishwa kuwa hii ni mara ya tatu na baadhi ya wafanyabiashara wamekiri kuwa huu ni mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya Maaskali polisi wa Kituo cha Msimbazi......"


Kwa masharti ya kutotajwa jina mfanyabiashara mmoja alikuwa na haya ya kusema “yaani hawa wazungu wamevamia hapa na Askari na kuchukua simu za kichina za Samsung wakati sisi mzigo tunanunua china hivi ni halali kweli ? Ujue Watanzania tunashushana na kutiana umaskini wenyewe kwa wenyewe ... hii ni mara ya tatu na kila wakija wanachukua mzigo wote hivi ni kweli serikali haijui ? au mpaka siku tuliwashe ndio watu watafutane au ijulikane? Au wanataka waseme tulianzisha vurugu , Raia wa kigeni aingie duka la mzalendo kupekua kweli jaman? Inauma sana unajua ?
Toka kwa Mdau aliye kula hasara mzigo wa SUMSANG sasa wao wanadai ni SAMSUNG
 
Wasi wangu ni pale mtakapokataa Polis nao wakatimiza amri ya Pinda mtakuwa na wakati mgumu
 
Mi yenyewe mshanichanganya. Kati ya sumsang na samsung au ni simsang... Ipi ya kichina
 
Kwa nini wachukuwe Simu tu? hizo TV feki hawazioni? MATAPELI tu hao
 
haya na mwingine huyu hapa nimemkuta mtaa za Aggrey anauza ndizi na kuku aina ya jogooo sijui kama nae ni Mzungu au laah maana sikumuuliza


 
Wanawaonea wananchi wanatakiwa kwanza wawashtaki TBS,TRA kwa kupitisha na kiidhinisha uuzwaji wa bidhaa feki
 
jamani sijaelewa.......wanachukuajechukuaje.....?....nia hasa ni nini......?
 
haya na mwingine huyu hapa nimemkuta mtaa za Aggrey anauza ndizi na kuku aina ya jogooo sijui kama nae ni Mzungu au laah maana sikumuuliza



Huyu si Mzungu.... labda ni Muhindi mwekundu
 
si kuna mamlaka husika zinazo chunguza bidhaa feki hapa nchini? Kwa nn haya yatokee? Yan hii serikali ni majanga kabisa aifai
 
SAMSING, SIMSING, SAMSANG, SIMSANG, SAMSUNGI, SUMSUNG, SIMSUNG na SUMSING zipo Kariakoo. Zooote feki, origino ni SAMSUNG ORIGINO. Tatizo moja tu, changa la macho.
 
kama ni hivyo basi na Apple waje haraka.....tunashindwa kuheshimiana huku mjini.........

kweli heshima imeshuka huku mtaani unamkuta PMOPP(Primitive Model Of Production Person) kashika mtekno af anakupiga bit m2 una nokia 6300
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…