Ayenda M
Member
- Jan 4, 2018
- 98
- 132
Salamu kwenu nyote!
Naomba nisianzie miaka ya 1990, kipindi ambacho ntakuwa natoa historia ya kusimuliwa au kusoma tu. Naanzia kipindi ambacho nilikuwa na uelewa mzuri wa mambo kwa kiasi fulani, naweza kutoa ushahidi nikiulizwa maana ninafahamu. Kumbukumbu zangu kwa leo zinaanzia mwaka 2004 kuja mpaka hapa tulipo 2020.
Arsenal ilikuwa imejaa watu haswaa, wale vijana wa kizazi hiki na wazee wetu wanamkumbuka mtu mmoja anaitwa Hleb! Hleb alikuwa fundi haswaa, ila akafanya kosa moja katika carrier yake ya kutaka kuihama Arsenal kwa nyodo tena bila kutaka kumuaga vyema mzee Wenger! Akatua Barcelona akiwa bado kinda kabisa, kilichofuatia akawa garasa na hakuna timu iliyomtamani! Akatua katika timu za level ndogo sana huko Spain na baadae akatoka na kuanza kupotea taratibu kwenye soka
Zile nyodo za Adebayor wakati anaondoka Arsenal, na maneno yake ya kejeli kwa mzee Wenger na timu nzima ya Arsenal nani anaweza kusahau! Akazidisha kwa kuwatukana mashabiki kwa ishara ya Dole la Kati baada ya kuifunga Hat trick Arsenal. Nadhani hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza na mwisho maana ameishia kuzurura tu katika timu mbali mbali na kuandamwa na majanga yasiyoisha
Huyu naye aliamua kujiongezea pesa ili aihame Arsenal na kwenda zake Barcelona. Akakosa nafasi na kurudi zake England tena na mara hii akitua Chelsea. Bahati kwake miungu ikamsamehe na akafanya vyema.
Huyu ni mchezaji pekee kipenzi cha mashabiki mpaka sasa pamoja na kulazimisha kuondoka. Muite Super FranCesc Fabregas! Mashabiki wa Arsenal huwambii kitu kuhusu huyu japo aliwakosea. Walipomsamehe mambo yakanyooka.
Kisa cha Sanchez sitaki kusimulia maana hata mtoto wa mshikaji wangu anakielewa vizuri! Vipi kuhusu Nasri, aliwatoa machozi mashabiki wengi wakati anaenda City? Japo sio kwamba kuhama Arsenal ni kujitafutia kuporomoka. Hapana.
Wapo waliohama vizuri na wakafanya vyema sana. Mmoja wapo ni mtukutu Cole. Vipi kuhusu Babu Chogo Henry? Kolo Toure? Ndio, ukihama kwa baraka utapata baraka pia na utafanya kazi za baraka huko uendako.
Mikasa hii ikanikumbusha mikasa ya WCB na baadhi ya wasanii wake! Kuna Tajiri wa Mavoko na Kijana wa Kimakonde! Hawa wamehama WCB, japo mmoja kaondoka kama Hleb alivyoondoka na mwingine kama FranCesc alivyoondoka pale Arsenal!
Tajiri wa Mavokali aliondoka Wasafi kwa mikwara kweli, akafika nje ya lebo akaachia ngoma na kwenda mabosi wa sanaa kujisajili akiongozana na dada yake. Akatamba kuwa ni muda wa kazi na watu kitaa wakasema tupe mambo, baadhi ya media zikampa kichwa naye akaona ameliteka soko kwa ngoma moja.
Sitaki kukumbuka kama ilifikisha Viewers aliowahi kuwapata akiwa Wasafi. Baadae waliompa kichwa wakaanza kumkimbia baada ya kuona mwana hawapi kile walichotajaria, na sasa hali si hali!
Sasa hivi kuna huyu kijana wa kimakonde, kasepa zake Wasafi huku kukiwa na mambo mengi nyuma ya pazia, katengeneza lebo yake maridadi! Kaachia Albamu fresh! Ila mpaka sasa sijui kama kuna ngoma ina watazamaji (Viewers) Mil. 3 na akiangalia vibaya yaweza imalize miezi 6 bila kufika viewers angalau Mil. 5. Hajakaa sawa kasaini msanii. Kama Jay Z vile siku hizi. Anavimba kwenye media.
Msanii wake aliachia ngoma na kama sikosei ngoma yake ya kwanza kama sio teaser ya ngoma iliwekwa kwenye youtube account ya Konde! Ilinichanganya ila nikasema acha niulize wataalamu wanisaidie! Bado sijapewa majibu ya kutosha.
Afrika sio Ulaya! Afrika sio Amerika au Asia! Afrika ni Afrika! Waafrika huwa tuna hulka. Konde inabidi afahamu kuwa waafrika kuwafanya wacheke ni dk sifuri ila wakiamua kununa hutaamini kama ndo wale waliokuwa wanakuchekea dk 1 iliyopita.
Aachane na kupambana na mtu, afanye kazi kwanza then mashabiki ndo watakuja wenyewe na watamshika mkono! Hata lebo ya Jay Z haikuanza kusaini wasanii na kufanya udhamini wa matamasha ndani ya siku tatu! WCB yenyewe Mondi ameitengeneza kwa miaka mingi tu, chini ya magenius wa biashara ya muziki Mzee Tale na Fella pamoja na Salam SK.
Lakini kumbuka kuna genius mkubwa wa burudani na bishara ya burudani Marehemu Ruge aliwahi kumshika mkono Diamond na WCB yake. Kwanini asifanikiwe. Mondi analinga kwa sasa kwa sababu hii. Jay Z anatamba now kwa kuwa hakukurupuka.
Sijasema wawili hawa wasingejitenga. La hasha! Walifanya jambo zuri. Ila kuna vitu walipaswa waulize na wajifunze taratibu kabla ya kufanya hayo. Ndo maana wazungu wanatuadhibu kila siku kwa udhaifu huu. Tunaona tunaonewa kumbe hapana. Tumechagua kujiadhibu na sio kuadhibiwa.
Wazungu wana msemo wao kuwa, "Ukitaka kwenda haraka nenda peke yako, ila ukitaka kufika mbali nenda na wenzako!" Waafrika tumejengewa utamaduni wa ajabu, utamaduni wa kusema kufanya kazi chini ya mtu ni utumwa na kumtajarisha mtu huyo.
Hayo ni mawazo ya ajabu sana. Ndo maana natamani somo la Historia lipitiwe upya ili ukweli uwekwe wazi kwa vijana juu ya mtazamo wa Utumwa. Ndo maana naonaga ni upuuzi mke kuachana na mmewe eti anamtesa, kila kazi anafanya yeye wakati chakula hanunui na maji hachoti yeye!
Kupika, kufua na kupiga deki? Unateswa hapo? Je, humuonei huruma mwenzio anayeamka usiku kwenda kusaka chakula? Na bado unasema hakujali! Unaachana naye. Una kichaa?
Dunia hii ina mgawanyo wa majukumu! Hauwezi kufanya kila kitu wewe, faida yote upate wewe! La hasha! Kuna kiasi lazima ulipe ili upate huduma fulani. Richie na Harmo nawaombea msizidi kuwa Sanchez kutoka kutoa assist 10 na magoli 17 ndani ya msimu mpaka magoli 3 na assist 1 ndani ya misimu minne! Wanaokupigia makofi leo ndio watasimama kukuzomea
Jumapili Njema!
Kwa maoni na Ushauri Nicheki Via Normal Text 0620275619