WCB, na wasanii wao wanatufundisha akili za kijinga na za kijamaa hazifai kwenye biashara

Randy orton

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2019
Posts
1,338
Reaction score
3,561
Diamond analalamika watu hawana shukrani wakati huo huo yeye aliwekeza na amepata faida kwa uwekezaji wake, hizo shukrani anazitaka za kazi gani!.

Rayvanny na Harmonize wanalalamika walikuwa wananyonywa wakati wanajua sana watu wamewekeza mamilioni kuwabrand na lazima waliowekeza wapate faida kwa uwekezaji walioufanya!!

Ifike kipindi hii mentality ya kijinga ya kulalamika uonewe huruma kwenye dunia ya ubepari ifike mwisho , WCB walipata na wasanii wao walipata sasa naona wote wanaogombania kuhurumiwa, upuuzi kabisa.

Wajaribu waone mikataba ya label kubwa duniani, unakuta msanii ni mkubwa lakini kazi zake zinamilikiwa na Sony Music na wala halalamiki ananyonywa kwa sababu anajua amefanya biashara na wakati huo huo hausikii Sony Music wakiomba shukrani kutoka kwa mtu kwa sababu wamefanya biashara.

2pac mpaka kufa kwake alikuwa amesaini mkataba kazi zake kumilikiwa na deathrow, Sony Music ndio kabisa wanamiliki hatimiliki za malegend wakubwa duniani ila hapa bongo sio label sio wasanii wote wanalalamika hovyo tu ili waonewe huruma.
 
Ana tabia asili za kibongo ile mtu akikusaidia iwe kidogo au pakubwa basi utakua mtumwa wake daima.

Ray na harmo walikurupuka kusaini mikataba mirefu tatizo elimu hawana. Hili suala walitakiwa wakae mezani na kuyaongea ila wamewaachia chawa wapige kelele na kuvujisha nyepesi nyepesi
 
Kama hawakusoma hayo sio makosa ya Diamond, ni wao wenyewe.

Pili ni biashara iliyonufaisha pande zote mbili, mi nawashangaa sana kuona wanacomplain wakati kila mtu amefaidika
 
Mtoa mada kwa upande wangu naungana na diamond anavyosema ni msaada kwasababu zipi hakuna jambo gumu kwa msanii kama kupata nafasi ya kuonekana na mziki wako kukubaliwa na jamii hasa kwenye kizazi hiki kilichojaa utimu na kiki zimepewa nafasi kubwa kuliko mziki na hii Ndio inasababisha wasanii wawe wale wale na ni wachache Sana wanatoa bila mgongo wa mtu kama Marioo kiufupi mazingira ni magumu kwa mtu kutoboa .Ukipita Youtube unakuta wasanii ni wengi mno na wananyimbo Nzuri lakini miaka nenda rudi hawatoboi pia kuna kuna kundi lingine wanafanya mziki nzuri lakini hawasogei hawapewi sikio la kusikilizwa mfano best naso n.k, uzi nyingi ninaona hapa zinafunguliwa kuhusu Ruby kwamba ana kipaji kikubwa lakini afanyi vizuri sokoni kwa wazungu wanawaiita Watu wa namna hii underrated artists ila wabongo halisia wanawaita wasiokuwa na nyota yuko wapi leo aslay? Vipi haya makundi ya wasanii niliyoyasema ikatokea wameenda Wasafi kwa mondi nae diamond akawa sign kwenye label yake kwa kuwapa mkataba after one year wakawa maarufu wa kutupwa utasema alifanya biashara pekee sio pia ni msaada? Sikwamba diamond kwamba anawafata ila wao ndio wanajipeleka kwake ndio the same as Rayvanny na harmonize.

Harmonize alitoka Mtwara hana mbele Wala nyuma hata uwezo tu wakumiliki baiskeli alikuwa hana akaja dar akafight Sana mpaka akaenda bongo star search wakamtema, akapeleka nyimbo zake radio mbalimbali zikawa azichezwi na sehemu nyingine anaambiwa quality ni ndogo atafute producer mkubwa afanye nae kazi ndipo siku Moja alivyosikia diamond anafanya show sehemu fulani akavamia akaonana nae diamond akamuomba amsaidie kimziki ikiwa diamond alikuwa hana hata wazo la kuwa na label kwa wakati huo baada ya harmonize kamn'gan'gania Sana diamond ndipo diamond akakubali na akamuwa kuwa na label akiamua kumgharamia muda wote harmonize yupo dar kabla ajamsign maana harmonize alikuwa anakaa kwa mshikaji baada ya hapo akamsign na akawa anabrand na akawa anajina kubwa hivi hapa huwezi kusema amefanya biashara na at the same time msaada maana kama ingekuwa ni biashara pekee sio msaada kwanini harmonize alimforce diamond awe msanii wake, kwanini asiendelea kufight kivyake bila kwenda kwa mondi?

Ukija kwa Rayvanny nae hivyo hivyo alikuwa pale tip top kakalishwa benchi na alikuwa kafeli form iv tegemeo lake ni mziki
 
Ukisema msaada inamaana haujanufaika .

Unawezaje kuita uwekezaji msaada?

Yaani mtu agundue sehemu kuna madini , achimbe madini , alipe kodi stahiki za serikali , apate faida halafu aseme amewasaidia ?
 
Kwani diamond anawafata au wao ndio wanamfuata?
 
innocent ebu soma mawazo ya mtoa Mada vizuri weka uchawa wa wcb pembeni mfano simple tu umepewa apo mtu kagundua sehemu Ina madini akawekeza kununua vifaa vya kisasa na kulipa kodi huo ni msaada?
 
Diamond analalamika watu hawana shukrani wakati huo huo yeye aliwekeza na amepata faida kwa uwekezaji wake, hizo shukrani anazitaka za kazi gani!.

Rayvanny na Harmonize wanalalamika walikuwa wananyonywa wakati wanajua sana watu wamewekeza mamilioni kuwabrand na lazima waliowekeza wapate faida kwa uwekezaji walioufanya!!

Ifike kipindi hii mentality ya kijinga ya kulalamika uonewe huruma kwenye dunia ya ubepari ifike mwisho , WCB walipata na wasanii wao walipata sasa naona wote wanaogombania kuhurumiwa, upuuzi kabisa.

Wajaribu waone mikataba ya label kubwa duniani, unakuta msanii ni mkubwa lakini kazi zake zinamilikiwa na Sony Music na wala halalamiki ananyonywa kwa sababu anajua amefanya biashara na wakati huo huo hausikii Sony Music wakiomba shukrani kutoka kwa mtu kwa sababu wamefanya biashara.

2pac mpaka kufa kwake alikuwa amesaini mkataba kazi zake kumilikiwa na deathrow, Sony Music ndio kabisa wanamiliki hatimiliki za malegend wakubwa duniani ila hapa bongo sio label sio wasanii wote wanalalamika hovyo tu ili waonewe huruma.
Wakilipa wakaondoka bila maneno maneno na kumchafua Diamond hana time nao.

Umeambiwa unataka kumiliki business yote peke yako lipia million 600 unaenda kumshtaki kwa Magufuli huoni huko ni kukosa shukrani? Okay Magufuli katazama reality kaona unapaswa kulipa mpunga...unaanza kuzunguka kwenye media kumtukana na kumuimba. Vijana hawana shukrani kabisa hao.
 
Hilo la shukrani ndio baya.

Diamond inabidi adai hela zake kwa mujibu wa mkataba, hakuna shukrani wakati wamefanya biashara.
 
Back
Top Bottom