WCB Waendelea kuchuniwa. Safari hii na mwanamuziki wa nje, Jason Derulo

gwa myetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
4,473
Reaction score
4,666
Kama kawaida jini mkatakamba gundu bado linaendelea kuwanyemelea lebo ya WCB ambao wameuanza mwaka huu vibaya kwa kugombana na Clouds media kitendo kilichosababisha nyimbo zao kusikiliza na michepuko yao tu huko Madale Guest house.

Kabla pia hawajaumbuliwa kuhusu biashara ya karanga ,perfume nk kuwa Domo ni balozi tu na si vyake.

Kabla hajapoa katika aibu hizo , akapokea rungu la kichwa kwa kuachwa na mzinzi na mzazi mwenzie Zaribosslady aliyechoshwa na skendo za huyo bwana ,ambaye alikuwa akibeba ukoo wake wote na kuupeleka South kumfanya bibie Zari ashindwe hata kupumua ,na ilifikia hata mama mkwe mama dangote kulazimisha kuvaa nguo za mkwewe, kwa kulazimisha apewe funguo za chumbani kwa Zari ili ajichukulie atakacho (ikiwamo kumwaga ulozi wake)·

Tukio la mahakamani kukatikiwa na malapa na mkanda wa boxer nayo haikuwa dalili njema kwake

Tuachana na hayo, juzi juzi Rayvany na Diamond walipost katika instagram zao wimbo wa Tip toe remix ulioimbwa na mmarekani Jason D ft Reyvavy cha ajabu mwenye wimbo hajapost hata kuuongelea wimbo huo ,lakini wcb kutwa wanaupost ,hapa kuna kitu Domo inabidi ajitathmini ,maana majuzi tu mwanamziki mwingine mmarekani Rick Rose aliamua kumchinjia baharini na kufuta post zake instagram.

Diamond unatakiwa kutubu, angalia unatumia muda mwingi kumpromote huyo Mboso lakini wananchi wamemkataa yeye na wasafi yako. Punguza ujuaji na hao mameneja wako kama vifurushi vya pamba maana unawaponza wasanii wako wasisikike redioni na tvs
 
Wengi mnamshambulia mtoa post mwisho katoa ushaur someni kwa makin nyie mnaosifia kila kitu ndo mnaopoteza baadhi ya nyota hapa nchini sio kila afanyacho ni kizuri mengine yafaa kupigiwa kelele ajitathmini sio malaika diamond kwamba hakosei lazima ukosokewe ili uwe bora.
 
Mbona kama umeandika mipasho?

Ila hao jamaa nao wanazingua sana.
 
Hakuna mkamilifu ukiangalia hayo matukio yaliyotokea kwake ni changamoto anatakiwa kuzifanyia kazi

Soma mwisho mtoa post katoa ushaur uwe mzur au mbaya kuna muda tujiandae kusikiliza hata mabaya na kuyapokea mkamilifu ni Mungu tu.
 
Technically speaking,hio nyimbo ni cover tu hivyo Justin utakuta hata hajui kama kuna mtz kafanya cover ya wimbo wake....as matter of fact kuna watu kibao waliofanya cover ya tip toe
 
Hakuna mkamilifu ukiangalia hayo matukio yaliyotokea kwake ni changamoto anatakiwa kuzifanyia kazi

Soma mwisho mtoa post katoa ushaur uwe mzur au mbaya kuna muda tujiandae kusikiliza hata mabaya na kuyapokea mkamilifu ni Mungu tu.
Hao wanaomshambulia wanajibu kile alichoandika mleta uzi maana robo tatu ya uzi ni kashfa na majungu robo ndio ushauri kwa hiyo lengo lake lilikuwa ni kutoa kashfa sababu ujumbe mzima upo kwenye hiyo kashfa
 
Hakuna mkamilifu ukiangalia hayo matukio yaliyotokea kwake ni changamoto anatakiwa kuzifanyia kazi

Soma mwisho mtoa post katoa ushaur uwe mzur au mbaya kuna muda tujiandae kusikiliza hata mabaya na kuyapokea mkamilifu ni Mungu tu.
Nilikusahau nilijua new comer nilitaka nimtongoze
 
Hakuna mkamilifu ukiangalia hayo matukio yaliyotokea kwake ni changamoto anatakiwa kuzifanyia kazi

Soma mwisho mtoa post katoa ushaur uwe mzur au mbaya kuna muda tujiandae kusikiliza hata mabaya na kuyapokea mkamilifu ni Mungu tu.

Asante kwa kunielewa lazima abadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…