WCB wako sahihi kuweka miaka 10 kwenye mikataba yao. Ni michache kwa uwekezaji wanaoufanya

WCB wako sahihi kuweka miaka 10 kwenye mikataba yao. Ni michache kwa uwekezaji wanaoufanya

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Nawasalimu kwa jina la Chama pendwa CCM.

Leo nami nimeona nitie neno kwenye hili suala linaloendelea mitandaoni na nje ya mitandao kuhusu mikataba ya wanamuziki kwenye label ya WCB.

Hii itasaidia watu wengine wasio na akili nyingi kama mimi kuelewa hili jambo. Maneno ya upotoshaji yamekuwa mengi sana.

Mimi nitajikita kwenye suala la muda wa mkataba, miaka 10. Wengi wanadai miaka 10 ni mirefu mno na inaashiria unyonyaji.

Mimi napinga na ninaona WCB wako sahihi. Kuna waliodai mbona Marekani na Nigeria mikataba huwa ni miaka michache kwanini hata Tanzania iwe mingi? Mimi nitajibu haya yote. Soma kwa makini.

Tukumbuke USA na Nigeria ni nchi za kibepari ambazo mtoto tangu akiwa mdogo anajua hapa hakuna cha bure lazima kupambana.

Kwahiyo mapema kabisa kijana anakuwa anajua yale mambo muhimu kama hatimiliki, mirabaha na kadhalika. Pamoja na kujua haki zake ila pia vijana wa hizo nchi za kibepari wanakuwa wanajua wajibu wao. Kwahiyo hata anavyopata bahati ya kusajiliwa inakuwa rahisi kwa mwekezaji kumnyanyua haraka msanii kwasababu kunakuwa hakuna mambo mengi ya kufundishana.

Isitoshe kwao kwenda kimataifa ni rahisi zaidi kwasababu ya kufahamu kiingereza vizuri. Hata wacongo nao wanapenya kimataifa kwa kujua vizuri kifaransa.

Tukirudi Tanzania utaona kwanza nchi yetu bado iko katikati ya ujamaa na ubepari na bahati mbaya mizani inaegemea zaidi kwenye ujamaa. Mfumo wa ujamaa ni mfumo uliozalisha wavivu wengi sana na ni mfumo ambao kiuchumi umeturudisha nyuma.

Huu mfumo wa ujamaa ndo utaona unawafanya WCB waone wanawasaidia wasanii na wasanii waone wao pale kwa ajili ya kusaidiwa na sio business.

Pia mara nyingi hapa Tanzania wenye vipaji vya hali ya juu ni wale vijana waliotoka familia za kipato cha chini kwahiyo ukimtoa mtaani/kijijini utakuta kuna mambo mengi sana unatakiwa umpe training. Kijana aliyeishia kidato cha pili shule ya kata lazima utamkuta na kasoro nyingi ikiwemo ya kutojua kiingereza wala hayo mambo ya hatimiliki.

Kibaya zaidi kwa sababu ya mfumo wa ujamaa akiwa anakuja mjini akili yake inamwambia anakuja kusaidiwa na sio biashara.

Utakuta kwenye kupambana angalau hata akisimama mbele ya watu awe na status ya kuitwa msanii inachukua hata miaka miwili. Hadi kupenya kwenye soko la ndani labda miaka mitatu au minne.

Na akishapenya ndani basi safari ya kumpeleka kimataifa huanza. Hapo ndo pagumu sana ambapo uwekezaji hutumia mamilioni ya pesa na muda mwingi. Kimsingi hadi mwekezaji kurudisha pesa zake sio chini ya miaka 10 au zaidi.

Mimi nashauri pande zote zijiweke mbali na lile neno KUSAIDIANA. Iwe business seriously. Kama msanii anataka kuvunja mkataba alipe hayo mamilioni yaliyowekezwa.

Miaka 10 hata kwa biashara zingine ni ya kawaida kabisa. Kupata pesa nyingi kwa miaka chini ya mitano hapa Tanzania ni suala zito mno, labda uwe fisadi.
 
kwa speech ile ya juzi yenye kilio ni dhahiri bwana diamond amewekwa kati kwenye rayvan saga 😀
 
Najikumbusha tu enzi zile mara ooh Ruge anatunyonya! Rest in peace! Saiz wao ndo wanyonyaji wakubwa
 
Najikumbusha tu enzi zile mara ooh Ruge anatunyonya! Rest in peace! Saiz wao ndo wanyonyaji wakubwa
Ruge sio poa. Sio wasanii tu hadi kina Eric Shigongo walishakutanaga na balaa la yule jamaa.
 
Back
Top Bottom