WCB,WASAFI Wanastahili sifa na Heshima Katika Bongo fleva.

Nedago

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2018
Posts
908
Reaction score
1,350
Habari ndugu wadau wa Jf,

Nikiwa napitia mitandao mbalimbali Jana
Nikaona tangazo la wasafi festival litakalo fanyika huko nchini Oman,mwezi wa nne.

Kwakweli nikafurahi kuona vijana hawa wa kitanzania wanavyojituma kutangaza muziki wetu wa bongo fleva kimataifa, tangu waanzishe hili Tamasha la wasafi festival mwaka Jana,

Tuliona jinsi lilivyotia fora ndani ya nchi kote lilikofanyika na hata katika nchi ya Kenya na bado hawajapoa wanazidi kulitanua hadi uko mashariki nk,wanafaa kuungwa mkono kwa hili,

Japo kuna watu wasioelewa watasema ni kwa maslahi yao,bila kujua ni hatua ya kusambaza muziki kuiacha kipato wanachoingiza,nimeona pia navy Kenzo wamekaribishwa kwenye festival hiyo ya wasafi huko Oman.

Hili ni funzo kwa lebo nyingine za muziki hapa nchini kujipanga na kuimarisha management zao na wasanii wao kufikia levo waliyoifikia wasafi na kuaanda matamasha makubwa zaidi ndani ya nchi ili kuongeza ushindani ndani ya nchi na hatimaye watoke nje Kama wasafi.

Maana Kama wakiachiwa wasafi tu, siku wasafi wakiteteleka na kupotea inaweza kuchukua muda tz kupata lebo kubwa Kama hii kimataifa especially Africa,maana kwasasa ni Kati ya lebo bora za kiafrika kutoka East Africa kwasasa.

Lazima wasanii wajifunze na wajipange kuwachallenge WCB wasafi wasiachwe peke yao,yasije kutokea ya kanumba na bongo muvi kimataifa.

Narudia tena lazima wasanii waache ubinafsi na kuongeza teamwork,lasivyo wataishia kupiga shoo za club tu na fiesta,na kuwaacha wasafi wakitamba ndani na nje,maana wasafi wao kila wiki wanapishana airport wao kwa wao,
Angalau na navy Kenzo na Vanessa.

The Future is in Our Brain's Tongue's and Hand's.
 
Hivi huyo Queen Darleen naye ni msanii na ana mashabiki kabisa? Mashabiki wake ni watu wa aina gani?
 
Hivi huyo Queen Darleen naye ni msanii na ana mashabiki kabisa? Mashabiki wake ni watu wa aina gani?
Hahahaha uyo kweli hafai ni kubebwa tu kisa yupo wasafi.

The Future is in Our Brain's Tongue's and Hand's.
 
Hili tamasha inabidi liahirishwe kwasababu ya kifo cha Ruge.
 
Hili tamasha inabidi liahirishwe kwasababu ya kifo cha Ruge.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Aiseee

The Future is in Our Brain's Tongue's and Hand's.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Utakuwa kichaa,Diamond akifa utakuwa wa kwanza kusema alisaidia kufikisha mziki wa Tanzania kimataifa.....na utawachukia sana kina Rich Mavoko wakisema walinyonywa na Diamond......WANAFKI SANA NYIE WATANZANIA WENZANGU.
 
Mbona mondi kapiga show Oman One man Army 2017,hiyi ya sasa hivi ni festival.AY kafungua njia lakini hajawahi kupiga katika matukio kama ya Mondi .Mondi kapiga show ya kutoa tuzo za mchazaji bora wa Africa mara mbili na Fainali za kombe la mataifa huru la Africa 2017 Gabon,hamna msanii TZ aliyewahi kufanya hivyo bila kusahau ufunguzi wa BET Africa,South Africa .


 
Ndo maana hii mijamaa mi siipendi! Yaani hapa nimechukia kishenzi na mihasira kibao! Sijui nikajimwagie maji baridi mwili upoe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…