Mkuu Pasco nimekupata sana na tupo ukurasa mmoja tatizo ni kwamba wabongo ni wajinga kiasi kwamba mpaka wale wanaotuamsha usingizini tunawapiga mawe, tunawabeza na hatuwaamini, matokeo yake ni kwamba na wao wanaamua kutu 'screw' zaidi kwa kuamua kuungana na wanaotu'screw'.
Kwa upande mwingine wale wenye uelewa (ambao wangeweza kutukomboa) wanakatishwa tamaa na hali hii na kuamua kuangalia maisha yao na familia zao. Tufanyeje????
.
Mkuu Mawazo Matatu, Tunahitaji uhamsho toka kwa watu wenye uwezo wa kuwa charismatic leaders ili itikadi ya mabadiliko iwaingie kama imani ya dini. Hii hali kuachana na harakati na kuangalia familia, ilishanikuta binafsi siku za nyuma, kwa kweli unakuwa frustrated familia inaangamia, na watu watakucheka.
Kama inside you, you are not oportunist, hata ukiachana na harakati na kuangalia maisha yako na familia yako, utaishi vizuri huku dhamira yako inakusuta.
Hata hivyo, Kitila Mkumbo alisema mahali, 'hatupaswi kukata tamaa', sasa tuko kwenye market economy ya uchumi wa soko, ili ufanikiwe kwa lolote, lazima uwe na nguvu ya kiuchumi ya kuwezesha uhamasishaji wa mabadiliko ya kweli. Hivyo kama huna nguvu ya kiuchumi, ni vizuri kujijenga kwanza ndipo kuingia na kustrike.
Nilisoma andiko fulani la Mzee Mwanakijiji kwenye his 'new year's resolutions' nikashauri ile 'cheche ya fikra' ingewekwa kwenye broadcast media, Watanzania wakatangaziwa ni nini kinachoendelea, wengi wangeamka.
Katika mapambano haya, ile formular ya 'if you can't beat them, join them' inaweza kuleta mafanikio kwenye CCM predominant ndio maana akina Mwanakijiji wanapojitambulisha kama wana CCM, halinipi taabu, sometime issue ni ukombozi na sio vyama, vyama is only the means.
Kwa vile mimi binafsi ni mwanaharakati at heart, ila sina nguvu za kiuchumi, nimetake a break for few years kujijenga ili kuepuka kuwa 'rugged trousered philanthropist', nikikamilika, nitaibuka, and will hit them very hard outside the box kwa lengo la uhamasishaji tuu wananchi walete changes na sio political office. 2010 is too near, too little, too late. 2015 will be the time.