We are the other people


Unashindwa kujibu hoja kwa hoja unaishia kutwist maneno, kuedit post zako na kuniambia nimeandika vitu ambavyo sijaandika, no wonder why hata hiyo biblia unashindwa kuielewa.

Nimeandika, Cain alimwomba Mungu, akikutana na watu wasimuue, wewe unasema nimeandika Cain aliomba asikutane na watu, kwa nini unapindisha maneno?

Halafu hayo maswali mbona huyajibu?
 
Last edited by a moderator:

Post hiyo hapo, haya sema sasa wapi nimeandika Cain aliomba asikutane na watu? Au utataka kuedit tena useme ulikosea?
 

Nimeiquote tena usije ukafanya editing zako,
kama huna hoja ya kujibu kaa kimya tu au go back to sunday school ukaanze upya, siyo kuleta ujanja ujanja wako hapa wa kupindisha kiswahili na kuedit vipost vyako
 
Last edited by a moderator:
Nilikuuliza swali kutokana na hiyo post yako, hukujibu ukauliza swali jingine, nimekujibu na me naomba unijibu swali langu Mkuu.
Kumbe wewe ndio mwana anthropolojia? Nilimuuliza mleta mada. waweza kujibu
 
Kumbe wewe ndio mwana anthropolojia? Nilimuuliza mleta mada. waweza kujibu

Hicho ulichomuuliza Mwanaanthropolojia kilitokana na yeye kujibu post yako ambayo uliniuliza mimi, mbona hukumuuliza kama yeye ni Mourinho?

Ungetaka kumuuliza yeye peke yake na akujibu peke yake ungemPM, kama umebandika hapa yoyote yule anaweza kurespond.

Unaacha kujibu hoja unaanzisha taarab, pathetic!
 
Mourinho ,sijui una tatizo gani,ila nimejifunza kuwa ualimu ni kipaji kikubwa na kinatakiwa kiheshimike sana,kwa maana huelewi kabisa,sijui una nini kwenye ubongo wako
'
Suala la Cain ni wewe ndo umelileta hapa sio mimi
'
Suala la "watu wengine" umelileta wewe sio mimi
'
Wewe ulisema Cain alimwomba Mungu akikutana na "watu wengine" wasimuue,mimi nikakujibu kuwa watoto waliozaliwa na Adam na Hawa hawawezi kuwa "watu wengine"?
'
Baada ya wewe na mtoa mada kuonekana kuilewa biblia tofauti,kwa maana kuwa Mungu aliumba watu zaidi ya Adam na Hawa,ndipo nikasema ni upotoshaji
'
Hapa ndipo nikakupa mfano wa binadamu kuanzia jiwe kisha mbwa halafu binadamu(isome vyema post yangu yenye mfano huu)
'
Bahati mbaya hukuuelewa mfano huo,ukafikiri nimesema wewe ndo umesema hivyo,ukweli ni kuwa niliupa mfano kukufanya ujue ni wapi sikubaliana na ninyi
'
Nadhani utakuwa umenielewa sasa!
 
Last edited by a moderator:

kwa nini yahweh aliumba mti wa katikati?
 

Sikutegemea any valid argument from you though,
"original sin" inakutesa bado ndio maana unabwabwaja na kupindisha maneno hapa,

'kajitakase' kwanza utokwe na hiyo original sin ili uwe huru kama sie "the other people"
 
Last edited by a moderator:

katika yohana 17;1-12
1. Yesu alipokwisha sema hayo, alitazama juu mbinguni, akasema, "Baba, saa imefika! Mtukuze Mwanao ili naye Mwana apate kukutukuza.2. Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uzima wa milele wote hao uliompa. 3.Na uzima wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.4 Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa nifanye.

yesu alipewa kazi gani ?
jibu lipo mstari wa 6."Nimekufanya ujulikane kwa watu wale ulionipa kutoka duniani. Walikuwa watu wako, nawe ukanipa wawe wangu; nao wamelishika neno lako.

kumbuka tunamuongelea yesu sio paulo,je yesu aliwahi kutangaza neno kwa mataifa?
hapana hakuwahi katika maisha yake yote kutangaza neno nje ya uyahudi, kama una ushahidi yesu aliwahi kwenda kwa mataifa kutangaza neno naomba unisaidie, kwamaana sijauona .kwa maana nyingine alipewa awatangazie wayahudi neno na wayahudi wote walimjua na walimtambua ila watu wa mataifa hawakumjua mpaka anakufa kwani hakuwahi kupewa watu wa mataifa hata siku moja


Yesu anatangaza achievements?
ndio na achievents zake soma mstari wa 6 na tunaposema achievemnts tunamaanisha alizofanikiwa kufanya akiwa hai na sio wakati umekufa,kwani huwez kusema umeachieve kitu wakati umeshakufa,na anajiipongeza assignments zake zote amezitimiza,na katika asssignments zake kuhubiri,na kuwaleta,kuwaponya watu wa mataifa haipo kwenye job description yake

katika mist
ari inayofuata anasema 7. Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetoka kwako.8. Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako, na wanaamini kwamba wewe ulinituma. 9. "Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea hao ulionipa, maana ni wako.

Je Yesu ni wa watu wote?
yesu hapa anakana kuuombea ulimwengu bali kwa watu wake ambao walikua wanafunzi wake wayahudi tu kwa maana nyingine watu wa ulimwengu,watu wengine hatuhusiki kabisa ,nashangaa kuna watu wanauombeaga ulimwengu kupitia yesu wakati yesu hakupewa hayo mamlaka na wala hatutambui

10. Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana ndani yao. 11. Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa,tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja. 12. Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea,isipokuwa yule aliyelazimika kupotea ili Maandiko Matakatifu yapatekutimia.

watu gani ambao yesu alikua nao na anawacha?

wanafunzi wake na wafuasi wake wengine wayahudi kwani hakua na mfuasi hata mmoja kutoka wa mataifa ,wewe na mimi hatukuwepo hapa anaongelea present na sio future,kwa maana nyingine hatuhusiki katika huo mstari huu ni mstari kwa wanafunzi wake

halaf kuhusu paulo,kwa kweli ni mtu wa mashaka ,mjanjamjanja,msomi anaejua kutwist maneno na akaweka sheria nyingi mpya ambazo kama hamjagundua ni yeye aliyeinvent uongo kwa mataifa
haaminiki kwani kila alipobanwa alikua yupo radhi kukana imani yake kuokoa maisha yake ingawa haikuweza kumsaidia mwisho wa siku.
so sion sababu ya kuangalia mistari ya paulo,kwan amekosa uaminifu atasema hiki kitabu hichi halaf atabadili hivi kitabu kile kulingana na mazingira, so i dont trust paulo na wala sikushauri kwani amepoteza authenticity
 
mwananthropolojia Ni kweli kuwa Yesu alilenga kuwaweka sawa watu wa israeli. Kwa ukweli wana wa Israeli tangu enzi za Musa hadi ujio wa Kristo. Shahidi ni wa haya ni maneno ya Stefano (utaniwia radhi nitaweka mwongozo tu). Mdo 7 Yote upate simulizi alilotoa Stephano mbele ya Kuhani mkuu dhidi ya ukaidi wa waisraeli.
Lakini ni Yesu huyu huyu aliyewatuma wafuasi wake akiwaambia waende ulimwenguni kote kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu...
Kadhalika ni Yesu huyu huyu kipitia Anania (Mdo 9:10-16), Paulo hakuwepo wakati Anania anapewa maagizo. Bwana anasema, Huyu (sauli) ni chombo kiteule kwangu Alichukue jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Naweza kununua hoja yako ya 'other people' lakini kusema kuwa hatuhusushwi na Kristo, na kwamba Paulo ni mwongo nakataa. Kama umeweza kuamini hoja ya other people kwa nini usiamini hoja za Paulo? Kama Petro alikabidhiwa Kanisa na Kristo, kwa nini Kristo alimwamnini wakati alimkana mara tatu? Ulitaka Paulo asiongope ili auawe mapema na kazi aliyopewa isitekelezeke?
 
Last edited by a moderator:
aisee najuta kufungua hapa leo. Kama hauko vizuri kiroho unaeza kufa kabisa kiroho.
 

suala la paulo lipo wazi kabisa ukisoma siku zake za mwisho mpaka kuwekwa gerezan,akiitwa mbel ya wayahudi anajifanya yeye ni myahudi anaefuata torati,akiwa na warumi anasema yeye ni wa Yesu na ni mrumi.
kwa kifupi Paulo alikua anajifanya kucheza na sheria(nadhani alikua mwanasheria),ujanjaujanja mwingi na kama Mungu anamruhusu huyo mtumishi aseme uongo ili aendelee na kazi za Mungu kuna maana gani Yesu na wanafunzi wake walipogoma kugeuza shingo zao na kusimamia imani zao mpaka dakika za mwisho?
kwani Mungu angeshindwa kuinua mtume mwingine aendelee na kazi kama Yesu alivyosema Mungu ana uwezi wa kuinua nabii hata kwenye mawe?
hakika nakwambia tusingemheshimu Yesu kama angekua kigeugeu.
hakika Paulo ni msanii
kuhus other people ushahidi wote unaonyesha hii dini haituhusu, habari zote wanajiongelea wao na sisi tunajarib kwa nguvu zote kutafta andiko litakaloonyesha sisi tunahusika kwenye hizi hadithi bila mafanikio
 
Raia Fulani hebu niambie hii kitu imekaaje kuhusu Peter mdo 10;10-16 ambapo peter anasikia njaa kali mpaka akapata kizunguzungu akaanza kuota vyakula vya kila aina mpaka haramu vinashushwa. njaa ikiwa kali hata mimi natamani nile chochote kilicho mbele yangu,mana alipokutana na watu wa mataifa fasta akaenda kuwaunga mkono ,akatoa hotuba ndefu sana badae wakamkaribisha kukaa nae .

ndugu zake habari zilipowafikia mdo 11;2-4wakamuuliza kulikon kwenda kujichanganya na wa mataifa na kukaa nao meza(kula) moja peter akaanza kujitetea.
ila kiukweli ilikua ni njaa haikua maono!

kwa kifupi mitume waliamua kujichanganya na watu wa mataifa baada ya wayahudi kuwakataa kwa maana kama ni kweli Yesu aliwaagiza waende kwa mataifa baada ya kufufuka mbona moja kwa moja hawakwenda kwa watu wa mataifa?

ni mpaka walipoanza kuuawa ,kutupwa gerezan ndio wakaanza kusogeasogea kutoa neno kwa mataifa, na bado walikua wanapingana.sasa najiuliza inakuaje mnapingana wakati bwana Yesu alishatoa maagizo muende kwa mataifa?

na njaa ilipozid wakasema vyakula vyote halali
 
Nimekusoma mkuu. Hivi Mungu alishindwa nini kuwavusha wana wa israeli pale jangwani kuwapeleka nchi ya ahadi kwa muda mfupi? Kwa nini watumie miaka 40? Mungu ana njia zake za ufanyaji kazi. Kadhalika mitume wa Yesu walikuwa ni binadamu ambao wana asili yao. Kumbuka mitume walikuwa wanamshutumu Yesu mula na wenhe dhambi lakini Yesu aliwapinga. Wana hisia za kibinadamu.
Ukisoma wagalatia2;16, 19-21, Paulo anawaambia wagalatia kuwa sheria zao za torati hazitawapeleka mbinguni. Palikuwa na sintofahamu wakati Petro alipopita Galatia na kusisitizaia sheria ndipo Paulo alkpopiga tena na kuwapa huo ukweli. Kwa hiyo tukjbali tu kuwa wale ni binadamu ambao walibahatika kutumiwa n Mungu kufikisha neno lake kwa watu. Tukubali pia kuwa maandiko yana majibu kwa maswali yetu. Unataka kusema leo hii Mungu wa Israeli hajishughulishi nasi? Hata mi wakati fulani nilikuwa na maswali mengi kuhusu nafasi yetu sisi mbele ya Mungu. Majibu mengi yapo kwenye mdo na nyaraka za mitume kwa mataifa mbalimbali. Mungu kaamua kutugeukia sisi. Tusiwe kama waisrseli ambao hadi leo wanamsubiri Masiha. Waisraeli wengi ni mayahudi na si wakristo.
 


Yeah_sure mkuu,...hata uislam/qouran nayo its not our story....tunajipendekeza sana kwa wayahudi na waarabu.
 
 
[ [[/COLOR]/QUOTE]

mmmmmmmmmmmh_hata sijaelewa...na pale nilipoelewa ninaishia kushangaa i.e iweje waisrael/wayahudi ndugu zake Yesu wamkatae mpaka sasa lakn kina yakhe kutwa kutoa mapovu mpaka kuuana.[/QUOTE]

Mkuu IGWE

Halafu kuna hii idea kwamba huyo mungu wa Israel baada ya watu wake (waisrael) kumkataa aliwageukia mataifa, kwanza sina uhakika na authenticity yake, sijui waliitoa wapi hii?

Ila inaibua maswali kadhaa,
huyu mungu wao ina maana hana msimamo?

Yaani watu wamataifa walikua na value tu pale alipotoswa na "Taifa lake Teule"?

Ina maana waisrael wasingemkataa mustakabali wa mataifa ungekuaje?
 

kuwa binadamu tunajua kuna pia kufanya makosa. lakini tuangalie nafasi zao katika jamii! kama hao walikuwa watu wa mungu kweli, basi walikua wanaongozwa na roho mtakatifu,na maamuzi yoyote yalikua yasifanyike bila kumconsult roho mtakatifu.na kama walikua wakimconsult roho mtakatifu haiwezekani wakakosea kwenye kutoa maagizo ya kiroho unless otherwise roho mtakatifu hakua nao kwaiyo walikua wakifanya maamuzi bila kumconsult roho mtakatifu.hii kupingana na kutoa maamuzi tofauti yaonyesha kabisa walikua wakiongozwa na utashi wao na si wa Mungu

suala la Mungu kutugeuka si kweli! ni kama nilivyosema wanaisrael wana Mungu wao na sisi pia tuna Mungu wetu,na Mungu wa Israel hajishughulishi na sisi,akijishughulisha na sisi, lengo litakua kututawala na kuwafanya watu wake waisrael wawe juu ya watu wengine wote.nadhani unafaham vita walivyozipiga na miungu na jamii zingine ili kuweza kutwaa maeneo na kuwatumikisha

maandiko ya biblia yana mafundisho mengi,kwetu inaweza kutumiwa kama reference book kati ya vitabu vingi,ila usife moyo kwani na sisi tuna Mungu wetu ambae nae anatenda miujiza na anasikiliza matatizo yetu.jaribu kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tz kuna maeneo ya maombi na watu wanaenda wanatatuliwa matatizo yao bila kupitia kwa Mungu waisrael.
tofauti kati yetu na wao ni kwamba sisi hatujawahi andika vitabu kuhusu Mungu wetu ila yupo hai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…