We live in a thought world! Ni kweli hiii?

We live in a thought world! Ni kweli hiii?

Nxt Millionaire

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
406
Reaction score
89
Mwandishi Wallace D Wattles anasema hatua ya mwanzo kabisa ya mtu kutajirika ni FIKRA, na kuwa twaishi katika dunia ya FIKRA, kwamba kila kilichofanyika chini ya jua chanzo chake kikuu ni FIKRA, anasema FIKRA ni nguvu pekee inayoweza kutengeza utajiri wa kuonekana,
Sina hakika ni wangapi leo hii tunaamini katika hili, kulinga na tafiti mbalimbali ni asilimia ndogo sana duniani, chini ya asilimia kumi wanaoamini katika hili na hakika hao ndo matajiri wakubwa duniani, jambo la kufurahisha ni kwamba wakati wowote, mtu yeyote anapokubali kubadili FIKRA na mtazamo wake na kuamini kuwa naye anaweza kutajirika bila shaka ataweza tu.


The First Principle in The Science of Getting Rich

THOUGHT IS THE ONLY POWER WHICH CAN PRODUCE TANGIBLE RICHES from the formless substance.
The stuff from which all things are made is a substance which thinks, and a thought of form in this
substance produces the form.


Original substance moves according to its thoughts; every form and process you see in nature is the
visible expression of a thought in original substance. As the formless stuff thinks of a form, it takes that
form; as it thinks of a motion, it makes that motion. That is the way all things were created.




Iwapo utapenda kupata nakala ya kitabu hiki waweza ni-PM au nitwangie 0716927070 au tembelea HAPA ujisomee.


Previous posts
 
mkuu mimi nazani tatizo c elimu ya vitabu ni udhbutu. HIVYO VITABU HAO WANAVIANDIKA KIBIASHARA NA NDO BIASHARA ZAO HIZO KUUZA VITABU.
KUNA DVD NA KUNA VITABU VINGI SANA BUT KAMA MTU HANA UTAYALI HAPO TUNADANGANYANA NA WENGI WALIO FANIKIWA NI WACHAHCE MNO WALIO SOMA HIVYO VITABU WAKAFANIKIWA WENGI WAMEFANIKIWA KWA KUDHUBUTU KWAO WAO WENYEWE. KAMA WATU HAWANA ENTRPRENERSHIP SPIRIT TUTAKUWA TUNADANGANYANA NA HIVYO VITABU.
VILE VITABU VIKO KINAZARIA ZAIDI NA UKIJA KWENYE PRACTCE YAKE MAMBO HUWA NI TOFAUTI, NA WALE MTU ASIKUDANGANYE NI BIASHARA ZAO KUUZA VITABU VILE.
MBONA BILL GATE HAJATOA VITABU VYAKE? KWA NINI HUJIULIZI NI KWA NINI?
 
mkuu mimi nazani tatizo c elimu ya vitabu ni udhbutu. HIVYO VITABU HAO WANAVIANDIKA KIBIASHARA NA NDO BIASHARA ZAO HIZO KUUZA VITABU.
KUNA DVD NA KUNA VITABU VINGI SANA BUT KAMA MTU HANA UTAYALI HAPO
TUNADANGANYANA NA WENGI WALIO FANIKIWA NI WACHAHCE MNO WALIO SOMA HIVYO VITABU WAKAFANIKIWA WENGI WAMEFANIKIWA KWA KUDHUBUTU KWAO WAO WENYEWE. KAMA WATU HAWANA ENTRPRENERSHIP SPIRIT TUTAKUWA TUNADANGANYANA NA HIVYO VITABU.
VILE VITABU VIKO KINAZARIA ZAIDI NA UKIJA KWENYE PRACTCE YAKE MAMBO HUWA NI TOFAUTI,
NA WALE MTU ASIKUDANGANYE NI BIASHARA ZAO KUUZA VITABU VILE.
MBONA
BIILGETI HAJATOA VITABU VYAKE? KWA NINI HUJIULIZI NI KWA NINI?

Yako maandiko yasemayo "yamtokayo mtu ndio yaujazayo moyo wake" Kwa maelezo yako Posho za Vikao liko neno ambalo umerirudia sana kuonesha msisitizo na kama hayo ndo yatokayo moyoni mwako bila shaka yatakuwa ndio yameujaza pia, na hizo ndo FIKRA zako.

Kumbuka = "THOUGHT IS THE ONLY POWER WHICH CAN PRODUCE TANGIBLE RICHES from the formless substance."

Sijui kama wadanganywa, wadanganya au wadanganyika na nini na nani, Wataalamu wa Saikolojia wanaifananisha tabia hii na WOGA, ambayo inakutwa kwa kundi la watu wanaotafuta USALAMA kwanza badala ya UHURU, (SECURITY CONSCIOUS).

Lakini kwako ndugu yangu nakutana na kitu kingine zaidi, UOGA ama wa Kusoma au kununua vitabu kwa sababu tu ni biashara, sina hakika ni vingapi uwa ununuagi kwa kuofia kwamba mwingine atakuwa anafaidika na wewe kununua, hili nashindwa pa kuliweka, kwa sababu nina hakika unafanyaga manunuzi ya aina fulani, unless uwe wajitosheleza kwa kila kitu, yaani unavyotumia unazalisha au kutengeneza mwenyewe, lakini kama si hivyo woga wa nini kununua kitabu kwa manufaa yako????

Hapo kwenye kijani sijakuelewa, ni nani huyo? labda wamaanisha Bill Gates wa Microsoft, je yeye kutoandika ni kigezo tosha? Huyu ni tajiri wa enzi zetu, je matajiri wooote waliwai kuandika vitabu?? Je kina J.P morgan, Henry Ford, John Rockefeller, Andrew Carnegie, nk waliandika wapi?

Wengi hawakuandika lakini walitoa mchango mkubwa katika vitabu vilivyoandikwa juu ya kujikwamua kiuchumi na mbinu zake, mfano Tajiri Andrew Carnegie ndiye aliyesababishwa kuandikwa kwa kitabu "Think and grow rich cha Napoleon Hill, bahati mbaya waogopa kununua na kusoma vitabu, lakini kitabu hiki ni kama mwarobaini kwa mtu anayetaka kutajirika kihalali, kina mahojiano, mbinu na mifano halisia toka kwa matajiri wakubwa kabisa duniani wa enzi hizo, kama nilivyosema bahati mbaya hutakaa ukisome kwa woga wa kuwa wengine wanafanya biashara.

Ulipo weye panaitwa "COMFORT ZONE" na Wataalamu wa uchumi, yawezakuwa panakufaaa maana yaonesha umeridhika napo, labda panaendana na ID yako, hongera.

Nina vitabu kadhaa, naweza kukuazima pasipo kulipa senti tano iwapo utaweza ondoa WOGA wa kusoma, ni twangie tu kwa namba hapo juu mara utakapokuwa tayari kubadili FIKRA au MTAZAMO.
 
Dah! I feel like i have not understood you...
 
Dah! I feel like i have not understood you...

That's a good sign of someone saying "tell me more", usiwe na shaka Ashadii, si yote uwa yanaeleweka mwanzoni ama yanaleta maana kwa kila mtu, lakini iwapo utaamua kwa makusudi kuyafuatilia ama kujipa muda kuyatafiti kwa kitambo kidogo mwishoni uleta maana, karibu sana.
 
Back
Top Bottom