We mbishi?

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
WAPENDA UBISHI watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao. Wakaamua kila mmoja AHADITHIE UBISHI aliomfanyia mkewe ili wapime nani kabobea zaidi kwenye fani.

MBISHI WA KWANZA AKASEMA
Mimi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilmpigia mke wangu simu usiku kapokea simu hakusema Haloo...Kulaleki! Na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi (haijakatwa)

MBISHI WA PILI AKAITIKIA
Mbona hiyo cha mtoto, mimi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lakini hakusema KARIBU mume wangu... aliniangalia tu.. nikaona analeta dharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu kazini.

MBISHI WA TATU AKAUNGANISHA
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mimi mke wangu tulipooana alikuwa anaona haya kunigusa... ananidengulia eti! Na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

MBISHI WA KWANZA NA WA PILI
Aaaaaaaaaaaaah! Faza! Acha usanii,nyie si mna watoto wawili lakini?

MBISHI WA TATU
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... kwani mimi nataka mchezo?!

Je wewe ni Mbishi Namba Ngapi?
 
Wote hao hawajielewi,,, ukifuatilia vzur maisha yao utakuta wataja kuishia wachawi!
 
Hao jamaa ni ma great poor thinkers...ingawa wana vijireason vyao
 
aaiiseee!!! Unakua na mume mbishi mpaka hajakugusa na watoto alea....lol...
 
Dah! Mkuu kumbe alikuwa anadondoshaga vichekesho anga hizi? Ila huyo mbishi wa tatu bonge la mjanja.
 

Ni ubishi au ubwege.? Huyo wa3 akajisalimishe mirembe.!
 
hivi huu ni ubishi au ni ghubu? huku ni kutaka kuthaminiwa na kunyenyekewa wakati wewe mhusika hujawahi kufanya hilo...
 
na wewe kama sio Mbishi, jiondoe JF ukiendelea kung'ang'ana na wewe ni mbishi vile vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…