Mleta thread anataka kufahamu je kwenye mabishano kati ya mwanaume na mwanamke nani anaongea kwa kasi zaidi na maneno mengi? Wataalamu wa lugha walikwisha tafiti masuala ya jinsia na lugha hasa kwenye mazungumzo (conversation) na kugundua kuwa wanawake wanaongea maneno mengi katika mada fulani na wanaume maneno machache sana; pia mara nyingi wanaoanzisha, kuongoza, au kubadili na kufunga mada katika hawa wawili ni mwanaume.
Kama unatilia shaka matokeo ya utafiti huu fanya observation - participant or non participant. Tena majibu mazuri yako huko uswazi, sasa sijui na elimu na ugumu wa maisha unamfanya mwanamke kuongea sana! Au hesabu maneno yaliyo kwenye mstari wa mwanaume na mwanamke kwenye hilo tangazo (10 kwa 16) na aliyeanzisha mada ni mwanaume. Tukipata teknolojia ya computer ya kurekodi 'ball possession kwenye mpira wa miguu, inaweza kutusaidia "words production and time taken" katika mazungumzo kati ya Adam na Eva!