Mwiba
Swali lako limekaa kiupendeleo pendeleo sana. Mimi sikubaliani nawe kwamba ni upinzani ndio utakao weza kuleta mabadiliko. Nilisikia wanachama wa CCM wapo milioni 4, upinzania sijui wako wangapi! Maana ya kujirudisha katika idadi ya watu ni ndogo kabisa, kwamba watu wanaoshiriki katika siasa za vyama sidhani kama wanazidi milioni 10. Kwahiyo, kunasilimia kubwa sana ya wananchi ambao hawapo kwenye siasa.
Mabadiliko yatakuja pale tu ambapo tutavunja kuta za siasa, udini, class, na kuongozwa na maslahi ya taifa. Hapa hatuhitaji viongozi wa siasa wa fanye nini, ila tunahitaji lengo la pamoja tufanye nini? Na tukikubaliana hilo kwa pamoja, viongozi wa siasa watakuwa na kazi yao ya kupiga makele katika ngazi za kitaifa, na sisi wananchi tutaendeleza vuguvugu la chini kwa chini! Kusema wanasiasa ndio washughulikie, ni unasema uwe ukombozi wakielite! Huu hautakuwa ukombozi wa kweli! Mambo yatakuwa yaleyale
Nionavyo mimi! Magazeti yaendele kuandika, jamii forum ibwabwaje, na cheche zitaendelea kuwaka. Mimi namatumain mabadiliko yanakuja. Maana mtoto wa binamu yangu mwenye umri wa miaka 7 aliniuliza, "hivi kwanini hawa mafisadi hawana aibu aunt!, mbona wanasemwa kila siku hawatoki! Kwanini hamwafukuzi! Hilo ni swali la mtoto wa miaka 7, ni dhahiri cheche za uelewa na kuhoji zimepandwa.