heaven on desert
JF-Expert Member
- Jan 25, 2013
- 1,025
- 393
Huwezi kumtumia Chameleon kuhalalisha ubora wa kiswahili. Kimsingi Kiswahili ni lugha ya taifa la Tanzania na itabaki kuwa hivyo. Hata hivyo, lazima tuone mbali. Katika soko la dunia ya biashara usomi na sayansi, Kiswahili hakina bao. Chameleon kama mwanamuziki asiyejua Kiingereza vizuri ulitegemea atumie nini? Wanaotaka Kiingereza kitumike mashuleni si kwamba wanapinga kuwa hakina maana. Kiswahili kinafaa kwenye nchi chache na maskini na kwa watu wachache kama Chameleon. Kama Kiswahili kingekuwa ndiyo msingi na chanzo cha mafanikio ya Chameleon basi wanamuziki wote wa Tanzania wangekuwa wamefanikiwa. Nadhani wakati Kiswahili ni lugha ya taifa, Kiingereza ni lugha ya dunia. Ni ushauri tu.
Sasa ndo kuishiwa hoja au...?? Matusi ya nini..?? Hivi wale mashoga na machangudoa waliofanikiwa kwa shughuri hiyo, unataka tuwaige kwa vile nao imewasaidia??wachina wanatumia hicho kingereza chako??
Ji**ga kweli wewe
Sio wote wa huko "majuu" wanatumia kiingereza kama lugha yao. Ni sisi tu tuliolewa kasumba za kikoloni ambao bado tunasujudia vya watu na kudharau vya kwetu!Kuna swala la kimtazamo na tafsiri.... Hwezi kukipuuzia kabisa Kiingereza. katika soko la dunia ya leo... kiswahili ni lugha ya Tanzania na ukanda unaotuzunguka.. lakini usidanganyike hebu nenda nchi za wenzetu huko majuu na hujui kabisa kiingereza ...lazia utachekesha na utaona dunia chungu... tuheshimu kiswahili chetu lakini kiingereza lazima kukifahamu kupambana na hali zote katika dunia hii
Hapo nadhani umechemsha!Huwezi kumtumia Chameleon kuhalalisha ubora wa kiswahili. Kimsingi Kiswahili ni lugha ya taifa la Tanzania na itabaki kuwa hivyo. Hata hivyo, lazima tuone mbali. Katika soko la dunia ya biashara usomi na sayansi, Kiswahili hakina bao. Chameleon kama mwanamuziki asiyejua Kiingereza vizuri ulitegemea atumie nini? Wanaotaka Kiingereza kitumike mashuleni si kwamba wanapinga kuwa hakina maana. Kiswahili kinafaa kwenye nchi chache na maskini na kwa watu wachache kama Chameleon. Kama Kiswahili kingekuwa ndiyo msingi na chanzo cha mafanikio ya Chameleon basi wanamuziki wote wa Tanzania wangekuwa wamefanikiwa. Nadhani wakati Kiswahili ni lugha ya taifa, Kiingereza ni lugha ya dunia. Ni ushauri tu.
Sio wote wa huko "majuu" wanatumia kiingereza kama lugha yao. Ni sisi tu tuliolewa kasumba za kikoloni ambao bado tunasujudia vya watu na kudharau vya kwetu!
Acha ulimbukeni. Hebu vile vile jaribu kupanda ndege ya Qatar Airways (hapa nazungumzia 787 Dreamliner) kama hujaelezwa kwamba lugha zinazotumika humo ni pamoja na Kiswahili pia. Uduni wa fikra utakuharibu milele!Hebu jaribu siku moja kupanda ndege aidha Ethiopia air line au ndege nyingine zinazokwenda majuu ... halafu uwe hujui kabisa kiingereza...
Wachina wameleta degree,na diploma ya Kichina Udom...usilete mchezo!wachina wanatumia hicho kingereza chako??
Ji**ga kweli wewe
Aisee UKI, tafadhali hebu fafanua hapo. Ni Ulaya gani hao wachina wamejaa kusoma lugha. Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, au...?ukweli utabaki pale pale english bado inatakiwa tujifunze tena kwa kasi ya ajabu kiswahili kinazungumza na watu wengi ukanda wa africa mashariki lakini ikumbukwe kuwa nchi ambazo ni masikini ikiwemo Tanzania tunajitahidi sana kushawishi foreign direct investment na hawa jamaa wanavyokuja lazima ujue jins ya kucommunicate nao kwa lugha kamwe hawawezi kujifunza hicho kiswahili, tungekuwa ni nchi iliyoendelea ambayo ina viwanda vyake hatutegemei wawekezaji waje kwetu hilo naweza kukubali tubakie na kiswahili chetu, kiswahili bora kibaki uraiani kama kenya walivyofanya sioni shida ila shuleni kingetumika english, china wanasema wanaendelea wanatumia lugha yao ila ikumbukwe kuwa sasa hivi wachina ndio wamejaa ulaya kusoma lugha...
Je vipi na Wajerumani (kwa mfano) nao wamejaa huko Uingereza kujifunza hiyo lugha? Umeandika mengi lakini sidhani kama yanao ushawishi wowote wa kile unachotaka kutilia mkazo! Swala litabaki pale pale: heshimu na tukuza utamaduni wako kama unataka kuheshimiwa hapa duniani. Kuendelea kutukuza Kiingereza na kudharau Kiswahili ni njia moja wapo ya kutufanya tuendelee kujiona duni maishani. Trust me, Bro, nipo huku "Ulaya" kwa miaka takriban thelathini na sioni ukweli wa hayo uyasemayo!mkuu university nyingi sasa hivi za uk kwa jinsi nilivyoona na wala sio kusimuliwa ukiangalia class wanafunzi wanaongoza kuja kusoma uk ni wachina na hii foundation class zilikuwa hazipo ila zimeanzishwa siku hizi special for chinese kusoma lugha then unaendelea kusoma degree yako au master yako, foundation za lugha 80% wanaosoma huku ni wachina...
Je vipi na Wajerumani (kwa mfano) nao wamejaa huko Uingereza kujifunza hiyo lugha? Umeandika mengi lakini sidhani kama yanao ushawishi wowote wa kile unachotaka kutilia mkazo! Swala litabaki pale pale: heshimu na tukuza utamaduni wako kama unataka kuheshimiwa hapa duniani. Kuendelea kutukuza Kiingereza na kudharau Kiswahili ni njia moja wapo ya kutufanya tuendelee kujiona duni maishani. Trust me, Bro, nipo huku "Ulaya" kwa miaka takriban thelathini na sioni ukweli wa hayo uyasemayo!
Sawa, nimekusoma. Tatizo ninaloliona ni lile la "wasomi" wetu kushobokea Kiingereza hadi wanashindwa kujieleza kwa Kiswahili ili kufanikisha mawasiliano na wananchi wa kawaida. Huu ni ulimbukeni chakari. Hapo hata hao Waingereza ni lazima watucheke!mkuu nahisi wewe ndio umenielewa vibaya kamwe sijazungumzia chochote kukidharau cha kwetu na kukiheshimu cha wageni mimi nimezungumzia pamoja na kufahamu lugha yetu vizuri ila lugha ya kiingereza nacho kina umuhimu wake mkubwa kwa ajili ya mawasiliano na wengine katika mataifa mengine na nilikuwa najibu hoja kuna mtu alisema china hawaongei english nikawa najibu kuwa hata wao wanajifunza english kwa nguvu zote ili waweze kuwasiliana na mataifa mengine. nikawa napinga viongozi kutuambia tuendelee na lugha yetu ilingali watoto wao wanawasomesha nje waanze wao na sisi watoto wa wakulima tutafuata, sijasema kamwe lugha yetu ni mbaya.