Wednesday, February 19, 2014 Harakati tanzania at 3:40 PM Vioja bunge la Katiba-Wajumbe wadai 300,00

Wednesday, February 19, 2014 Harakati tanzania at 3:40 PM Vioja bunge la Katiba-Wajumbe wadai 300,00

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,053
Reaction score
3,259
Licha ya watanzania kulalamikia matumizi
mabaya ya fedha za umma kupitia bunge la
katiba ambako kila mjumbe analamba sh
300,000 kwa siku hivyo kumaliza bunge akiwa na
sh milioni 21.Lakini leo katika moja ya vikao vya
wajumbe,wengine walalamikia kiasi hicho
kwamba ni kidogo mno. wanataka kiongezwe.
Mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo Julius
Mtatiro anasema kuwa kwakweli baadhi ya
wajumbe wenye uchungu na nchi
wanashangazwa na wenzao wanaotaka kiasi
zaidi ya laki 3.
Hapa chini ni andishi lake.
"Tunafahamu kuwa kuna njama zinapangwa ili
wajumbe wa bunge la katiba ati waongezewe
fedha zaidi.
Hoja hii imetolewa leo hii na mmoja wa
wajumbe huku ikionekana kuwa maarufu na
inayoungwa mkono na baadhi ya wajumbe, hasa
wabunge wa CCM.
Binafsi na wenzangu wengi tumepanga kutumia
kila uwezo kuzuia nia hiyo OVU, ifikie wakati
tuambiane ukweli vinginevyo nchi hii watu
watakufa masikini.
Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku
zinatosha kabisa, ambaye hazimtoshi aongeze
za kwake, na ambaye anaona hawezi kuongeza
zake aondoke Dodoma ili kupisha wanaoweza
kutunga katiba kwa posho ya shs 300,000
waendelee.
Laki tatu tunazopata zinatosha kila kitu na
CHENJI inabaki, zinatosha kula, kulala, kumpa
dereva na kuishi Dodoma.
Lazima sisi tunaotunga katiba tufahamu kuwa
maisha ya wananchi ni muhimu na kwamba
wana mahitaji yasiyokwisha hata baada ya
bunge hili.
Baadhi yetu tulioko humu bungeni tutakataa
jambo hili kwa maneno na vitendo. Wakipitisha
kwa wingi wao tuta-boycott kuzipokea.
Kenya pale mnakumbuka hoja ya wabunge
kujiongezea mapesa ilipingwa vikali na
wananchi waliandamana hadi nje ya ukumbi wa
bunge. Hapa Tanzania hata zikiongezwa milioni
kila siku hutaona mwananchi anachukua hatua
kwa vitendo, kuoneshwa kutoridhishwa kwake.
Tuna tatizo kubwa sana, sisi viongozi na
wananchi wetu. Kuna mtu anasema, viongozi ni
zao la jamii hiyohiyo.
Tuungane pamoja kusimamia jambo hili, ninyi
mlioko nje na sisi tulioko ndani."
 
nngejuaje kama ipo ... na sikuiona ...
ZZK ndio kichefuchefu chako ww ..

Pimbi wewe utakurupuka vipi kuanzisha thread kabla ya kulikaguwa jukwaa husika? ₩

Kama huyo mshirikina ndio chocolate kwako mpe akufumue.
 
Pimbi wewe utakurupuka vipi kuanzisha thread kabla ya kulikaguwa jukwaa husika? ₩

Kama huyo mshirikina ndio chocolate kwako mpe akufumue.

u got small brain to settle some small issues .. .
na ndio maana CHADEMA kinaitwa chama cha wanywa Viroba .. ni kwa ajili ya watu wachache kama nyie .. mnakiharibu chama ..
kwan ni lazima kuangalia na kuona .. kama sikuona kulikua na ubaya wa mm kuiweka iwepo .. na je isingekuwepo ..
JF kuna idara ya watu wanaofanya filtation za thread ..wakiiona wataitoa if topic is duplicated .. si kasi yako . act like a man
 
kama wao wanasema 300,000/: kwa siku haitoshi je, na anae pokea hyo hela kwa mwezi inakidhi mahitaji yake?
 
duuuu! lak 3 kwa cku haztoshi? Na wale wanaolipwa laki 3 kwa mwezi wasemeje? its not fair kabisaaa
 
Back
Top Bottom