Weekend siku ya jana nilikwenda kufanya masaji chimbo jipya

Weekend siku ya jana nilikwenda kufanya masaji chimbo jipya

kinyamkela mahaba

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2022
Posts
1,178
Reaction score
1,596
Khali za uzima jamani

Jana baada ya kutoka job mida ya saa kumi jioni nikaenda chimbo jipya kwangu kwa ajili ya masaji. Home niliona ni mapema sana kurudi.

Kwa kweli dsm ni pana mno mno mno.
Basi nikakaribishwa na kuingia ndani. Nilikuwa na 50000 mfukoni.

Nikanyoa nywele kwanza then nikapelekwa kwenye chumba cha masaji.

Kabla ya hapo kinyozi(dada) akaniambia kuna ukoko kwenye nywele nikakumbuka dar kuna joto so akanipaka dawa flani kabla ya kunyoa.

Mule ndani nikavua nguo nikabaki na taulo. Ila nataka nijue kitu kimoja. Why ukishazifua wanazitupa tu kwenye meza means hakuna utaratibu mzuri?

Walipokuwa wakinisugua mgongo waka stop wakasema nina mafuta na joto jingi hivyo nikaoge kwanza.

Ikabidi nikaoge kwanza kabla ya kuendelea. Nikatumia dk 2 tu chap.

Kisha nikajikausha na kuendelea na masaji. Walinisugua sana.

Mpaka saa 2.5 nikawa nimetakata sasa.

Wakaniambia maji niliyotumia ni mengi na muda ni mwingi mno so nikawalipa 50000 tu kishkaji.

Nikachukua nguo zangu nikavaa huyooo home huku nikimeremeta.

Usiku huo niliburudishwa na mauno mwanana ya Haika mke wangu mdogo mtarajiwa.

Jamani tusiache kwenda masaji. Ni kwa wanaume kamili tu.
Vijana msikate tamaa siku moja mtafika hapa nilipofika
 
Umelipa kitu cha 50k kwa ajili ya kusuguliwa tu!
 
Wenzetu pesa za kuspend ovyo ovyo hivi mnatoaga wapi? Unampa mtu more than 10k ili akusugue sugue tu na kukupaka mafuta!!! Acha nibaki na ushamba wangu tu...
Ukiishi Kwa kuona 10k or 100k nyingi basi utabaki hivo hivo, pesa ni vile unaichukulia ndio itakavokuja na hutoigopa kuitumia. Pesa ni mentality brother vingine vyote ni results tu za pesa. Mtu unaweza ukawa na 20k tu mfukoni ila usiogope kunyoa saluni ya 10k sababu you have An abundance mindset na mwingine akawa hata na million akalalamika kulipa 3k kwenye kunyoa.
 
mwingine akawa hata na million akalalamika kulipa 3k kwenye kunyoa.
mimi ndio huyo sasa. Naweza kua na millions ktk account lkn nanyoa uswahilini tu. Kinyozi wangu ni yule yule tu miaka nenda rudi ana banda lake la mbao, mashine moja, na vispirit vya kusafishia na vipoda, nanyoa kwa buku mbili na natoka fresh.

Nilishawahi zama barbershop kali, jamaa wakanichonga chonga ovyo ovyo, zaidi niliishia kunawishwa maji ya uvugu vugu na binti mrembo na kupakwa scrub na maneno matam, elfu saba ikachomoka shwaaa! Sikurudi tena. Priorities tu!!!
 
😂😂😂daah mi siwezi tatizo sio pesa ila ile kushikwashikwa na mtu simjui itanipa tabu sana asee anii. asa unasuguliwa mwili mzimaa au ni mgongo tu...???
 
mimi ndio huyo sasa. Naweza kua na millions ktk account lkn nanyoa uswahilini tu. Kinyozi wangu ni yule yule tu miaka nenda rudi ana banda lake la mbao, mashine moja, na vispirit vya kusafishia na vipoda, nanyoa kwa buku mbili na natoka fresh.

Nilishawahi zama barbershop kali, jamaa wakanichonga chonga ovyo ovyo, zaidi niliishia kunawishwa maji ya uvugu vugu na binti mrembo na kupakwa scrub na maneno matam, elfu saba ikachomoka shwaaa! Sikurudi tena. Priorities tu!!!
Ndio Ile story jamaa wa mbeya aliyeua, jamaa kamuua mtu wa parking kisa 7000 ya parking wakati gari yake ni Hilux 2016. Imagine mtu tajiri lakini 7k anaona ni pesa nyingi sababu ana scarcity mentality. Mwengine ana IST tu lakini angempa 10k huyo wa parking na chenji angemuachia. Pesa tuzienjoy ila tusiziabudu.
 
Ukiishi Kwa kuona 10k or 100k nyingi basi utabaki hivo hivo, pesa ni vile unaichukulia ndio itakavokuja na hutoigopa kuitumia. Pesa ni mentality brother vingine vyote ni results tu za pesa. Mtu unaweza ukawa na 20k tu mfukoni ila usiogope kunyoa saluni ya 10k sababu you have An abundance mindset na mwingine akawa hata na million akalalamika kulipa 3k kwenye kunyoa.
Nimejifunza kitu hapa
 
Back
Top Bottom