Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Eyakuze ni mmoja kati ya Waafrika watatu pekee kwenye orodha hiyo na mmoja kati ya 11 ambao hawako katika utumishi wa serikali.
Taasisi ya Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) inayoshughulika na utawala bora na Apolitical, zimemtambua Eyakuze kwenye orodha ya watu 50 wanaohamasisha maboresho na mageuzi ya kiutawala baada ya mapendekezo ya wataalamu, utafiti kufanywa kwa waliopendekezwa na baadaye mapendekezo hayo kupitiwa na taasisi ya WEF.
Washiriki huchaguliwa kutokana na sifa mbalimbali za uongozi zikiwamo: Kuweka msisitizo kwenye matokeo, ubunifu na kufanya majaribio, pamoja na uhusiano na wadau kijamii, kitaifa na kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na TWAWEZA kwa vyombo vya habari jana ilisema, Eyakuze alichaguliwa kama mmoja wa watetezi bingwa wa wananchi wa kawaida.