Serikali ijikite katika kufanya Tanzania kuwa moja ya mataifa duniani yenye wajenzi bora kabisa, ( hii ifanyike BILA KUDHALAU FANI NYINGINE), Kwa kuanzia;
1. Iliunde upya shirika la nyumba la taifa (NHC) ili lijikite katika kutengeneza nyumba za kuishi, shule na majengo mengine yaliyo bora kwa gharama nafuu. Hii inawezekana!
2. Ilifufue shirika la MECCO ili lijikite, kwa kuanzia, kutengeneza barabara za mitaani na mifumo ya maji ya mvua.
3. Itenge na kupima maeneo sahihi ya kujenga miji mipya yenye kushirikiana na miji ya sasa kila mkoa.
4. Itenge fungu la fedha (kwa mkopo au kutoka bajeti ya maendeleo, n.k. ) ilikuanza ujenzi wa miji iliyopangwa na yenye kiwango kwa kupitia NHC na MECCO, TANESCO, TTCL n.k.
Ujenzi holela usinamishwe mara moja, ni hasara kwa taifa.
5. Lengo ni kuhakikisha Tanzania yote imejengwa kwa mpangilio.
- Nyumba zinazotengenezwa ziuuzwe/zipangishwe kwa wananchi.
- inawezekana kuwa na nyumba bora kwa gharama nafuu kwa kuwa;
a. Madirika husika yatanunua material ya ujenzi kwa wingi na hivyo kuwa na nguvu ya kupata kwa bei ya chini.
b. Lengo halitakuwa kupata faida kubwa, ila itakua kuhakikisha pesa of nayowekwa kwenye mradi haipotei au kupungua thamani.
n.k.
Faida za kufanya hivi.
1. Maisha bora kwa wananchi kwa kuwa na makzi bora.
2. kwa kuwa huu utakua ni mradi mkubwa wa nchi nzima, na endelevu, utaleta ajira nyingi zilizo rasmi. Ajira wakati wa ujenzi na kwa kupitia ukarabati endelevu.
3. Sasa italeta ulazima wa kuanzisha au kuboresha viwanda vinvyotengeneza vifaa vya ujenzi.
Ikiwa ni pamoja na kuchimba chuma na kutengeneza bidhaa zake kama nondo, misumali n.k.
4. Wananchi wasio na fani za ujenzi, mf walimu, madaktati, wakulima, n.k. watajikita katika kuwa wazuri katika kazi zao ilikuweza kununua/kupangisha nyumba bora, ukilinganisha na hali ya sasa ambayo wanalazimika kujua ujenzi ili wasimamie ujenzi wa nyumba zao ambazo nyingi zinakua chini ya kiwango.
kumbuka ni ndoto ya karibu kila mmoja wetu kumiliki nyumba bora, je sote inabidi tuwe wajenzi?
5. shirika kama Posta litaweza kusambaza huduma mpaka majumbani, kwakuwa miji ikipangwa ni rahisi kuweka anuani za nyumbani. Mashirika mengine kama ya mawasiliano na usafiri n.k yatafaidika pia.
5. kama taifa tutaluwa uwezo mzuri wa kijenzi, na kwakuwa tumezungukwa na nchi ambazo hazijajengwa kwa mipangilio mizuri, basi tunaweza kujenga na huko kwa faida. Pia tutauza vifaa vya ujenzi huko pia.
6. Huko mbeleni MECCO itaweza kutanuka na kujenga barabara kuu na madaraja n.k.
7. kwa kujenga wenyewe bila kumtegemea mchina, mkorea n.k Tutakuwa chimbuko la kumnyanyua mtu mweusi ambaye kwasasa anadharailika duniani kama mtu maskini na asiyejiweza kiakili kama wengine. Kwa hali ya sasa tunamtegemea sana mchina kwa ujenzi..
tujue kwa wazungu walijenga kwao, wachina wamejenga kwao, tusiwe tofauti, na sisi tijenge kwetu.
8.n.k