Weka In Case Of Emergency (ICE) kwenye simu yako ya mkononi endapo utapata tatizo wasamaria wema waweze kuwasiliana na watu wako wa karibu

Wengi wetu leo tunapenda kuweka Password kwenye simu zetu ambayo inafanya iwe ngumu kwa mtu kuitumia ikiwa kuna hali mbaya imekupata kama kupoteza simu, magonjwa, ajali au hata kifo.

Lakini kwa maarifa haya madogo nitakayoshiriki, labda tunaweza kujiokoa sisi wenyewe na maisha ya wengine pia.

HATUA YA 1
Wakati simu yako imefungwa, kawaida huonyesha nenosiri (password). Chini yake, utaona dharura (Emergency). Bonyeza dharura, kisha utaona habari za dharura. Bonyeza habari ya dharura (mara 2) Utaona kitufe cha penseli upande wako wa kulia, bonyeza juu yake kuhariri(kuandika taarifa zako).

HATUA YA 2
Kisha ingiza anwani unazotaka kuhifadhi kama dharura inapokupata. mfano: unapoishi, namba za simu za watu wako wa karibu mfano (mama baba, kaka, rafiki, mke, mume, dada) Unaweza kuweka namba nyingi iwezekanavyo. Sasa namba hizo ulizohifadhi zinaweza kupigwa/kupigiwa kupitia simu yako hata wakati simu yako imejifunga kwa password, bila hata kuingiza password yako.

KUMBUKA:
Ili kupiga simu bonyeza palipo andikwa dharura (Emergency) na nambari zilizohifadhiwa hapo zitatokea. Unaweza kupiga nambari hizo bila kufungua simu.

Nafsi inaweza kuokolewa kupitia hii.
JISIKIE HURU KUSHEA NA WENGINE Huwezi kujua, KUSHEA KWAKO kunaweza kuokoa maisha ya mtu.

Asante.
 
Hii inahusu watu na nchi zilizostaarabika. Sisi watu wanaibia wenzao waliopata ajali, waliolewa na kupata matatizo mengine.
 
Safi sana nishawahi kutana ba ajari mtu kafa simu yake iko locked
 
Wengi wetu leo tunapenda kuweka Password kwenye simu zetu ambayo inafanya iwe ngumu kwa mtu kuitumia ikiwa kuna hali mbaya imekupata kama kupoteza simu, magonjwa, ajali au hata kifo...
[emoji1531]
 
Katika maisha ya sasa hivi ni kawaida mtu kuweka PASSWORD kwenye simu yake ili kulinda na kudhibiti matumizi asiyopenda watu wafanye bila idhini yake...
Njia hiyo hiyo kwa nchi zenye watu wasio staarabika hutumia kubypass frp kwa android huoni kuwa ina side effects
 
Mtanzania mwenzangu kama unasoma thread hii weka nambari za dharura kwenye simu yako sasa hivi. Fanya hivyo tu itakuja kukusaidia badae kukitokea dharura, watu hawatahitaji kufungua simu yako ili kuwapigia ndugu zako kuwapa taarifa.

Utakuwa umewarahisishia kazi kwa kubofya maandishi yaliyoandikwa emergency na namba uliyoiweka itajitokeza na kupiga simu ambayo inaweza kuokoa maisha yako.

Simu yako ukiwa umeilock, Kuna maandishi ya Emergency Call ya click then weka namba za watu wako wa karibu....kama ulishafanya hivyo Good for youView attachment 2279106
 
Wazo zuri ila Sio simu zote zina feature hiyo mzee
 
Wazo zuri ila Sio simu zote zina feature hiyo mzee
Smartphones zote ziko nazo. labda hizi simu ndogo...na sidhani kama Kuna watu wanalock simu ndogo za batani
 
Asante mleta mada kwa kunifundisha hili. Sasa hivi nimefanya kwenye simu yangu na imefaa.

Haya mambo madogo madogo lakini yenye umuhimu ndio yameendelea kuwafanya wazungu kuwa mbele kimaendeleo kuliko sisi tunaopuuzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…