Weka Picha za Magari ya Leyland Tanzania

Weka Picha za Magari ya Leyland Tanzania

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Leyland ilikuwa ni brand kubwa sana ya magari mazito ya kiingereza kuliko Scania, Benz, na Fiat enzi hizo.

Yale magari ya Leyland CD (Clydesdale) na Leyland (Albion) yalikuwa hayashindwi mlima au matope kwenye sehemu yoyote Tanzania wakati barabara zetu zikiwa mbovu sana.

Hayakuwa na spidi kubwa sana lakini yalikuwa stable sana; yaani yalikuwa yanatumia injini ya nguvu sana na suspension yake ilikuwa siyo ya mchezo mchezo.

Mabasi yote ya kupitia milima ya Kitonga wakati huo yalikuwa ni Leyland. Isuzu zote zilikuwa zinaishia korongoni. Kumuuzia mtu tiketi ya usafiri wakati huo ilihusisha pia kumwambia kuwa basi lako ni Leyland CD.

1738377333410.png


Ghafla magari haya ya Leyland (original) yakapotea na kuishia kuwa Leyland Ashok ambyo siyo ALbion au CD.

Kama una picha ya gari la Leyland (CD) au Leyland (Albion) Tanzania iweke hapa tujikumbushe.
 
Hawa watengenezaji walikwama wapi? maana gari zilikuwa bado zinatesa sokoni pamoja na wenzao NISSAN DIESEL.
1980_Leyland_Boxer_(33052316681).jpg
 
Back
Top Bottom