MSIMULIAJI
Uliwahi kuhisi harufu ya kifo!!!
Hivyo ndivyo majasusi wawili wasiojuana walivyohisi. Hakuna aliyependa kuishi maisha hayo, japo kila mmojs alijikuta katika maswali,mateso, mawazo yasiyokuwa na mwisho.
John Truck, huyu alikuwa jasusi ambaye alitumiwa katika kumtafuta dakitari ambaye alikuwa ametengeneza kirusi ambacho alitaka kukieneza katika jiji la kampala. Waganda walitambua kabisa kuwa John Truck ni jasusi, na walitambua jinsi ambavyo Jonh Truck anamjua dakitari huyo ambaye amedadisiwa na kutambua kuwa anaishi marekani.
JohnTruck ni ni mzaliwa wa Tanzania, mama yake ni mhindi na amekuwa akijishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya. Baba yake ni mtanzania mzaliwa wa bukoba kagera kashai na amekuwa akijishughulisha na wizi wa madini na kazi amemfundisha mwanae. Babu yake ni mzaliwa wa bukoba kashai huku bibi yake akiwa mzaliwa wa bukoba vijijini kule kasharu.
Pia, John truck alikuwa mrefu mithiri ya wanyarwanda na alifanikiwa kuibeba sura ya baba yake ambaye alikuwa na rangi ya kiafrika. Anapenda kuvaa suti nyeusi akibadili rangi ya shati na tai bluu na nyekundu. Ana mwili mkubwa ambao ulikuwa umejaa vya kutosha kutokana na mazoezi makari.
Kutokana kuwa baba yake John Truck amekuwa akifanya wizi wa madini, hilo lilimfanya anakuwa na pesa nyingi. Kutokana na kuwa na pesa nyingi sana hilo lilimsukuma kumsomesha mwanae wa kwanza aliyemwita John.
Truck hakumsomesho mwanae ali akapewe kazi selikarini, bali alimsomesha ili kufuta visingizio vya iwapo mwanae ataanza kazi ya ujasusi akikamatwa apate majibu rahisi na haraka. John amesoma vya kutosha japo hana faida na elimu yake maana anaitumia kama pambo la ndani. John hajawai kuwa na rafiki wala mpenzi, maana alipofikisha miaka 18 baba yake alimwelezea mambo kwa undani kuhusu kazi atakayoifanya hapo mbeleni. Kwaiyo Truck alimpa mwanae njia ya kufuta marafiki na wapenzi,
Kuanzisha visa visivyo na maana.
Kampala, Uganda
Huku John Truck akiwa amekaa kwenye kiti, simba yule alizidi kusogea kumwelekea mmoja kati ya wale watatu walobaki. Akailamba pua yake akitumia ulimi uliokuwa mrefu na mwembamba. Anapomaliza anakitisa kichwa chake huku akiupanua mdomo wake ulokuwa na meno manne makubwa na marefu na mazuri yalimaliza chuo kikuu cha ulaji wa nyama.
Simba yule alimsogelea aliyekuwa na vidole viwili. Akautoa ulimi wake na kuanza kuulamba mwili mateka yule. John Truck alikaa macho wacho wazi tena kwa umakini mkumba akitizama jinsi gani simba humtafuna binadamu. Macho yake yalitelemka na ulimi wa simba yule maana hakuwa kuona igizo kama lile.
Simba yule alizidi kuulamba mwili wa yule mateka. Akiwa makini alishtuka alianza kugeuza jicho lake moja kumwelekea mtesaji kama paka aliyekula panya aliyekufa kwa kusu. Akigundua mtesaji hayuko makini na igizo lile, bali yuko maini na hisia za John. Akaanza kulielewa igizo lile lililo chezwa tangu apo awali.
Gafra yule simba alimg'ata mgongo na kuanza kumburuza kuelekea kwenye mlango aliotokea simba yule. Na baada ya kuingia ndani mlango ulifuna wenyewe. John alifurahishwa na igizo hilo maana amefanikiwa kuuelewa mcheza kidogo. Sikutambua john alikuwa akiwaza nini.
Mtesaji akamuuliza John Truck: Jitetee, au bado utasema utakapofikiwa wewe. John Truck alimtazama mtesaji yule kisha akamwambia: aka bado, maana bado sijaridhika na igizo ili na lililopita, ebu nipe linalofuata maana napenda nifike huko chini kwa dakitari. Mtesaji alikasirika sana kutaka kuutoa uhai wa John Truck. Sauti ilisikika "iwe sebo".
Alishusha pumzi.
Yule mtesaji aliitoa simu yake, ngeli ya simu janja na kuanza kuandika ujumbe fulani, huku John akizidi kuendelea kumtazama mtesaji yule aliyekunja sura yake mithiri ya nguo za mitumba. Kisha aligeuza macho yake kwa yule aliyekatwa mdomo, alijikuta akizidisha tabasamu lake maana jamaa yule hawezi kununa.
Mlango wa juu ulifunguka. John Truck alifurahishwa na mtambo ule uliofunguliwa na vyuma vikubwa vyenye meno. Akiangalia mtambo ule wenye meno kama picha ya programu ya simu ijulikanayo kwa jina la mipangilio (settings). John akajiambia "nimewaweza".
Ule mlango ilipofunguliwa ukatokea ngazi, kupitia zile ngazi akaonekana mwanajeshi akishuka akiwa amevalia sare ya jeshi la Uganda. Alipofika chini akasogelea mtesaji yule alikuwa mweusi sana hii ikizidi kumthibitisha kuwa huko uganda. Yule mwanajeshi akamtazama mtesaji yule pia naye akamtazama wanaongea kwa signo za uso. John aliwatizama tu akitaka kujua wanasema nini. Jambo hilo lilimwondoa uoga.
Walipomaliza kupeana alama hizo, yule mtesaji akaenda kwenye ukuta na katika ukuta huo kulikuwa na bayana zenye michoro ya vitufe. Akaenda na kubonyeza barani yenye kitufe cha mstari. Na hapo kamba zilikuwa zimetoka John Truck zikakimbia na kupotelea ardhini hivi kwamba visingeweza la kulikuwa na kamba kwenye kiti kile.
Yule mwanajeshi akamwambia John Truck: nifuate hewe mateka. John hakujibu jambo lolote,alichofanya aliamka na kuanza safari ya kumfuata mwanajeshi yule alionekana kukomaa zaidi ya yule mtesaji japo alikuwa na mwili mdogo, ila yeye hakuwa machachari, alikuwa ametulia na alionekana kuwa makini sana.
Walizopanda ngazi na wakatokea chumba cha juu. Wakafuata mlango waliutumia kuingia pale mwanzo. Wakatoka, safari ikaendelea na bado John Truck alizidi kuyatazama mazingira yale kwa umakini mkubwa. Akazidi kuyasoma na kuyakamilisha mazingira yale. Safari ukakolea kwenye chumba namba 100.
Yule mwanajeshi akamwonesha Johnstone John Truck ishara ya kuwa atangulie mbele. Huku mlango ulifunguliwa, huku moyo ukienda mbio maana mlango ule una mchoro wa kutisha karibu na ile namba 100. Akaingia ndani, akamtazama nyuma akamwonesha yule mwanajeshi alivyomtazama. Yule mwanajeshi alikuwa na kovu lilishindwa japo lilikuwa tayari limekauka.
Kiotomatiki mlango unajifungua . Bila kuchelewa John Truck aliligeuza shingo lake na kutazama mbele, tena makini mkubwa. Akajaribu kusogea ingawa bado hakuweza kuona kiumbe chochote kwenye kile chumba.
Chumba namba 100.
Chumba kile kilikuwa kikubwa sana kilichoonekana kuwa na madirisha ingawa yalikuwa yamefungwa. Kilionekana kuwa na mlango mmoja yaani wa kuingilia tu. Kilikuwa sakafu iliyoonekana kuchoka huku kuta zake zikiwa na plasta huku mwanga hafifu wa taa ndogo zilizojitupatupa kama nyota za hasubuhi.
John Truck alizidi kukichunguza huku akizidi kuangalia kama kutakuwa na kiumbe chochote katika chumba kile kinachoogopesha na kuzishutuwa hisia. Atimaye akafanikiwa kumuona kiti kilichokuwa na muundo wa kufungwa na kufunguliwa. Akakisogelea kiti kile akamtazama kwa makini akainama na kukichunguza chini naye akajiakikishia kuwa kiko salama, japo hakukikalia. Akautumia mda ule kukichunguza chumba kile kikubwa na chenye ukimya ka kilichotelekezwa.
Katika chunguza chunguza akagundua kuwa kuna kamera iliyolingana na sindano na yenye mwonekano Kawa sindano, ingawa haikuwa na sehemu ya kuchoma. Hapo ndo kulikuwa na kamera.
John alijifanya kama hajaiona. Akaingia na wazo maana alijuwa jinsi ambavyo wanaona vyote anavyofanya, akaamua kugeuza tabia yake na kujitoa katika hali ya ujasusi na kujifanya kama mtu aliyetoka kijijini akishangaa mataa ya mjini. Akaanza kujifanya anashangaa mwonekano wa zile taa na hapo ndo alitambua kuwa zile taa pia ni kamera. Hapo ndo alimweshimu mganda.
"Habari yako John Truck". Ni sauti ilitokea nyuma yake. John Truck jakugeuka haraka haraka, bali aligeuka polepole na kugundua kuwa sauti ile ile ilitokea kwenye spika iliyokuwa imeningizwa kwenye roof (paa). Akaitazama spika ile kwa sauti ya dharau "niwe na habari gani, badala ni nikuulize habari. John Truck aliamua kumfukuza adui wa wengi ambaye ni uoga na akayatamka maneno yale huku akiwa ameota zama spika ile.
Ukimya ukapita bila jibu lolote
ENDELEZA WAZO . ..... .................