Kuna rafiki yangu aliniambia kuwa mti unaozaa machungwa unaitwa mchungwa na mti unaozaa maembe unaitwa mwembe(muembe) lakini mti unaozaa ndizi unaitwa mgomba kwa sababu ukipanda ndizi hautaota mgomba je hii ni sahihi?
Mmhh hapa mtihani, mimi nakumbuka kuna ndizi zina mbegu, na nimewahi kusoma kwamba unaweza kupanda mgomba kwa mbegu za mgomba ambazo zimo ndani ya ndizi, hivyo ni kusema Si Sahihi, kwamba mgomba lazima upande shina.
Naomba fungua kiambatanishi hichi kina maelezo na picha, kusibitisha maelezo yangu, Banana
Ama hilo la Mdizi kuitwa mgomba ntalifanyia kazi kwa wazee.
kama hujaridhika nipo kwa mjadala zaidi