Wekeza kwenye fikra / maarifa; huko ndo kunakosemekana kwamba hakuna uharibifu wowote

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,598
Iko hivi:

Wazo la mradi / biashara likitolewa na mtu ambaye hana mtaji - pesa - (star-up capital) huonekana kama ni upuuzi. Sio kwamba huwa ni upuuzi bali upuuzi huwa ndani ya anayelipokea wazo hilo. Wazo lenyewe huwa liko pale pale na thamani yake iko pale pale na likifanyiwa kazi linazaa matunda mema. Hivyo upuuzi ni ndani ya anayelipokea.

NA PIA

Mtaji (Pesa) kwa ajili ya mradi / biashara (Star-up capital) alio nao mtu ambaye hana wazo lolote ni kama makaratasi. Sio kwamba thamani ya mtaji huo haipo bali ubovu wa thamani ya mtaji huo upo ndani ya mmiliki wa mtaji huo.

Hivyo katika hali zote mbili mwenye kukwamisha maendeleo ya sehemu yoyote ile ni yule mwenye umiliki wa mtaji (pesa) pasipo kuwa na akili za kuifanyia kazi.

Jiulize: Una wazo lolote au una mtaji pesa.

Wekeza kwenye fikra / maarifa; huko ndo kunakosemekana kwamba hakuna uharibifu wowote ule (hata Biblia inaweka ilo wazi) ila kwenye vitu vya kuonekana kuna uharibifu wa wazi.

Ni kwa nini pesa huondoa uwezo wa mtu kufikiri?
 
Ni kwa nini pesa huondoa uwezo wa mtu kufikiri?
Premise ya hii sentensi ina assume kwamba ina ukweli..., Sio kweli kwamba Fikra ni inversely proportional na Pesa
 
Bora kuwa na wazo( maarifa) juu ya jambo fulani kabla ya kupata pesa, kuliko kuwa na pesa ndo utafute nini cha kufanyia
 
Fa
Premise ya hii sentensi ina assume kwamba ina ukweli..., Sio kweli kwamba Fikra ni inversely proportional na Pesa
Fanya uchunguzi utakubaliana nami, chukulia hata wanasiasa kabla na baada ya uchaguzi au uteuzi.
 
U
Bora kuwa na wazo( maarifa) juu ya jambo fulani kabla ya kupata pesa, kuliko kuwa na pesa ndo utafute nini cha kufanyia
Uko sawa
 
Mkuu uko vizuri sana. Nimesoma mara tatu hii hoja.
 
Fa
Fanya uchunguzi utakubaliana nami, chukulia hata wanasiasa kabla na baada ya uchaguzi au uteuzi.
Pesa haiondi uwezo wa mtu kufikiri, bali achievement, au kupata kitu alichokuwa anataka kunaweza kupelea kubweteka na kutokuona umuhimu wa kuweka juhudi zaidi..., sio pesa tu, bali ni achievement.., ukweli ni kwamba reaching the top might be hard, but maintaining it is even harder..., hata kwa upande wa pesa kama ulikuwa big fish kwenye small pond basi ukipata pesa unapanda daraja na kukutana na bigger fish unless ukitaka kubaki in the same pond i.e. ukiridhika....

N:B: kumbuka naongelea statement yako hii kwamba ni void...
Ni kwa nini pesa huondoa uwezo wa mtu kufikiri
 
Pesa siyo msingi wa maendeleo, falsafa ya marehemu Mwl JK Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo siyo pesa wala wazo, tatizo ni kukosa utulivu wa akili. Ukiwa na wazo, wazo la biashara lina mchakato mpaka kufikia hatua ya kuwekeza ktk hilo wazo, wazo kwa mara ya kwanza linaweza kuwa ni zuri kimtazamo lakini ukilipeleka ktk utekelezaji likashindwa kufanikiwa na kuna wazo laweza kuwa baya mwanzoni lakini ktk hatua ya kuatamia (incubation) likaja kuzaa matunda mazuri. Kwahiyo hapa ni utulivu wa akili kutokuwa na haraka ya kuingia ktk biashara bila ya kuwa na mpango biashara na kufanya mchakato wa kutosha kabla ya utekelezaji.Ukiwa na pesa tulia kwanza usikurupuke


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…