Ni kweli, lakini namna ya udikteta ni lazima ili maendeleo yapatikane...Tanzania tuna raslimali nyingi pengine kuliko nchi nyingine barani Afrika, lakini maendeleo yetu yako chini kwa kuwa tuna leadership inayoogopa kuchukua hatua muafaka za kuleta maendeleo....Watu wenyewe wa Tanzania nao ni wavivu, wapika majungu, wana wivu na wanataka vitu vya 'dezo'...utamaduni wetu ni mbaya kabisa kuhusu utendaji wa kazi..kwa Tanzania mkwepa kodi anasifiwa...mwizi kwenye kampuni anasifiwa..usipoiba kwenye kampuni au taasisi wakati una nafasi nzuri wengine watakuona wewe ni mjinga...nafasi za uongozi Tanzania ukipata tunaziita 'mwenzetu ameuchinja', na kwamba 'atakula bata'...Mtanzania akiteuliwa uongozi anafanya 'party' au sherehe kujipongeza kwamba sasa 'umaskini umemtoka'...Watanzania wako tayari kuchangia kwenye michango ya 'harusi' na siyo maendeleo ya kusomesha watoto..hakuna mahali hapa Tanzania utaona watu wachangishana kusomesha watoto wao...Yaani wanachangishana kwa anasa na ufahari...Kiongozi akiwa mkali kwenye kampuni au taasisi anapikiwa majungu na kuondolewa...Kiongozi anayezingatia kanuni na taratibu kwenye taasisi anaitwa mnoko na ambaye hafai na lazima ahamishwe...Sasa Rais wetu JPM anakejeliwa kwa kuitwa 'dikteta' kwa kuwa anataka taratibu zizingatiwe...wanasia wetu ni wanafiki wa kutupwa wawe wa CCM au upinzani wote ni wanafiki tu...shutuma za ukiukaji wa haki Haki za binadamu hapa kwetu Tanzania ni dhidi ya serikali tu na vyombo vyake...Ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na vyama vya siasa vya upinzani kama kuwamwagia watu tindikali inaonekana ni sawa tu...Watanzania tufanya au kupiga hatua ya maendeleo tu ikiwa tutabadili mindset zetu za utendaji wa kazi na uwajibikaji ndani ya jamii...JPM anataka kuleta mabadiliko ya kweli lakini bado watu wamemzunguka na wameapa kumkwamisha , ushahidi ni teuzi za ma-DC na ma-DED ambapo kilichotokea ni uchuro kwa kuwateua baadhi ya watu wasio na sifa za uongozi wala taaluma...Watanzania wengi wanapiga kelele za demokrasia lakini hata maana ya demokrasia hawajui...wanadhani demokrasia ni kuwatukana viongozi...