Wema amlipua Kajala kisa unafiki

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu ( 25) aka mama ubaya, amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ' K' ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.

Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho ; ' Kajala : Wema mnafiki' . Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ( 25) Katika habari hiyo , Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala ( Dacutee) .

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar , Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.

"Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ' ok fine' na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu - wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa , alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana' ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao? "Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie , itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi ? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake ? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu- wish hajammaindi?" aliwaka Wema .

Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine .

"Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu ( waandishi ) kuhusiana na tatizo letu , si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya, " alisema Wema .

Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni , Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala , hakusita kufanya hivyo .

"Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea , niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala , " alimalizia kusema Wema .

Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana' ke , kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.
 
Ndo nashangaa binamu, we acha tu huyu mama ubaya haelewekag, kesho atakwambia ana miaka 24

Mmmh..binamu hii kali ,,watu hawakui umri ila sura zinazeekea.yetu macho sie
 
Mama ubaya bana, kwa hiyo hiyo picha na kajala aliombwa apige na nani?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huyu msichana anapenda sana kuandika kwenye magazeti,hana hata lamana nyumba yakukaa hana kazi ufahari...........
 
Kajala si angepiga kimya kwanza wema kafuliaa, kajala angemrudishia zile milioni ....halaf akaachana nae au kuna kingine wanalazimishanaa ninii
 
Kajala si angepiga kimya kwanza wema kafuliaa, kajala angemrudishia zile milioni ....halaf akaachana nae au kuna kingine wanalazimishanaa ninii

Wema anamuonea wivu kajala, maana siku izi ana pesa hatar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…