Wema amzaba makofi meneja wa hoteli

Verdy CB

Senior Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
149
Reaction score
66
VIOJA VYA DADA YETU VINAENDELEA

WEMA AMZABA MAKOFI MENEJA WA HOTELI

DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe,Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.
Wema Sepetu.

MAELEZO YA MENEJA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.

WEMA, WENZAKE WAZIDIWA NA KILEVI
Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki zake walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.

Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.

Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani?

WEMA AANZA KAZI YA KUSHUSHA KIPIGO
Aliongeza kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.

¡°Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.¡±
Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO. Hadi tunakwenda mitamboni, Wema anasakwa na polisi ili apandishwe mahakamani.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja.

Hata hivyo, Kanumba aliamua kuifuta kesi hiyo kwa sababu ya kutaka amani. Wakati huo Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe.

ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alilikwaa soo jipya, akakamatwa na Polisi wa Oysterbay na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ¡®Bob Junior¡¯.

Katika kesi hiyo, Hakimu Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema na kumhukumu kwenda jela miezi sita au faini ya shilingi elfu arobaini ambapo alilipa feha hizo. Wakati huo, Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ¡®Diamond¡¯.

SOURCE: GPL
 
Safi sana wema wanyooshe hao wasio na heshima
 
Mmh! Huyu mlimbwende wenu ni kichefuchefu,Ana nguvu nchi hii!! Kama nani? Au wakuu wanapoingiaga kwenye naniii yake huwa wanabakiza mamlaka humo?
 
Wajua ukifanya fujo na matusi huwa wana file na kupigwa pia!ili alipe fidia kubwa ya uharibifu!sidhani Wema anaweza akampiga vibao visivyo na idadi mwanaume au kijana hata wa miaka 12!
 
isije ikawa Mediterranio na konyagi zao ndogo za shilingi elfu ishirini na tano
 
aisee goodluck kuyumbu ila jina la hotel hakuna
kamchapa vibao khaaa
mie tu bibie tutachapana inakuwaje yeye achapwe?
Wema asubirie kisanuke tu atalia sana
 


Huyu meneja mzushi kudai kapigwa vibao visivyo na idadi na demu tena aliyezidiwa na pombe !akiri ndogo hii

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
hivi kuna mwana jf apa wa kiume anaweza kubali apigwe vibao na wema visivyo na idadi? uyo meneja ni. mini kabaang nini
 
Huyu meneja mzushi kudai kapigwa vibao visivyo na idadi na demu tena aliyezidiwa na pombe !akiri ndogo hii

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

labda alikuwa anatafuta ushahidi.....
 
Mie nilidhani kuwa jina la hotel ndo lilikua la muhimu zaidi katika habari kuliko la huyo meneja butu.
 
Bila kuuandika wema hawawezi kuuza. Kwa style hii mke na watoto wake wataweza kwenda toilet.
 
Cjawh kupigwa vibao na mwanamke ever..by the way..ijumaa wikiend+shigongo=udaku+
 
Ingepatikana picha ya huyo meneja Kuyumbu ingesaidia kutupa picha ya meneja anayeshusha hadhi ya wanaume kwa kupigwa na Wema au alijilegeza makusudi ili alipwe?
 
Mwanamke mlevi.....kumchapa mtu halafu akaenda polisi....
 
Huyu dada yenu naye bado hajielewi kama serengeti wake dayadomo,,,


Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
meneja yesu kweli ningekua mimi nishakata funua zamani
 
mmmmmmmmmmmmmmmmmh....huyu jamaa atakuwa punga,...achapwe vibao na mwanamke halafu analemaa na kukimbilia kuita polisi,...mimi nilifikiri wema ndio angekuwa ameenda kufungua jalada polisi akiwa na ngeu na hatamaniki,....ni mjinga huyu
 
meneja yesu kweli ningekua mimi nishakata funua zamani

Yeah mkuu....lakn wanaangalia wa kumzingua,...kuna kissister duuh fulan hapa arusha kilitaka kuleta za kuleta eti nacho kinajifanya kimaarufu hapa mjini...si kikasea njia kikatuletea ngebe maeneo ya bugaluu...nilikishikisha adabu vibaya yeye pamoja na vibana pua vyao vikaloa...kuja polisi watu hatupo...pumbaaafuuuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…