Wema aonyesha jeuri ya pesa nchini China

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa
na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita , Wema Sepetu ‘ Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China.

Chanzo makini kilicho ‘ kloz ’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini , kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la
Fiesta, akiwa ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake , Martin Kadinda na Petit Man , wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo.

Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo ,Wema na wanaume hao wawili walichukua
vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn ,
inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China.
“Yaani Wema jamani ana mambo,
inavyoonekana lile rhumba la wakati ule ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho
inauma .

Wewe fikiria mtu amekwenda
kuchukua vifaa vya biashara , unakwenda na
hao wanaume wa kazi gani kama siyo kupoteza fedha tu , ” kilisema chanzo hicho.

Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi kuliko yoyote duniani , ni ununuzi wa vipodozi , kwani ana mpango wa kufungua duka kubwa
katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi maisha ya starehe , wakila bata katika klabu
mbalimbali za usiku , ambako
wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha.

“Kwa matanuzi anayofanya kule , hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana , angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli , angetafuta tu hoteli ya kawaida ili kubana
matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa ,
tena na wanaume wawili wanakutegemea , hizo pesa si kuzitapanya tu jamani , ” kilisema chanzo hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo.
 
Vipodozi from China???haya wadada wa mujini mkae tayari madame analeta mali....chezea mkongo keshawezesha wewe???
Alisema alipewa mtaji na ndomo akala bata...huu utakua wa mkongo tu...
 
Itakua vyema kuanzisha biashara yake halali asisahau na sabuni za kubana K suport tutampa kubwa tu
 
Itakua vyema kuanzisha biashara yake halali asisahau na sabuni za kubana K suport tutampa kubwa tu

Vipi kwani na wewe una tatizo nini shoga angu???
Labda kama unamaanisha zake yeye
 
Vipodozi from China???haya wadada wa mujini mkae tayari madame analeta mali....chezea mkongo keshawezesha wewe???
Alisema alipewa mtaji na ndomo akala bata...huu utakua wa mkongo tu...

Atakua amefuata biashura cyo biashara mtaji kiuno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…