Naona aliyepewa kazi ya "kuigiza" sauti anamtaja Steve hapo mwisho kuwa amechoka "kurecord" hii "episode"
Hii yote ni kazi ya mikono ya Steve Nyerere!!Atarudije mjini na kuendelea kukaa bila kujua kodi ya nyumba inatafutwaje?ni kutumika na hawa wanasaisa wa siasa za kuchafuana
Chadema nao wanajibu mapigo kwa kumchafua Mwenyekiti wa Chama dola,tena kwa kashfa kubwakubwa sana....Hawa vijana tunaowalea kuwa viongozi wa baadae tunawapa misingi ya hovyo hovyo hovyo sana sana.Misingi ya siasa za kuchafuana mitandaoni.
Vijana wametengeneza magroup ya WhatsApp fake,na wengine nao wakajibu kwa magroup fake
,
Yaani kwa mtu uliyewahi/uliye karibu na hao wanaoonekana kuwa ndio walikuwa wanajiandikia hizo msgs,utajua tu huu ni uongo.
Nina miaka zaidi ya kumi nikiandikiana Msgs na Lissu na Mdee,iwe ni kwa e-mail au SMs,huo sio uandishi wa Lissu wala Mdee.Kwa jinsi nilivyozoea kuandikiana nao Msgs,eti Lissu anaandika "Eee bwana"??Huyu sio Lissu hata kidogo
Hata huo uandishi wa Polepole ni wa kuigiza!!Kuanzia alieanza na "voice note" mpaka hawa wa "screenshot" ni upuuzi mtupu
Tunaandaa vijana wa hovyo kabisa.
Hivi mnafikiri Mwalimu na "uadilifu" wake hakuwa na mpango wa kando!?Hivi mnadhani kina Kawawa walikuwa Malaika??Hivi mnadhani hao kina Bhoke Mnaka na kina Sozingwa walikuwa Malaika?Lakini mbona sisi vijana wa zamani hayo mambo tulifundishwa kuyaweka kwenye koo na kifuani ili yasifike mdomoni na kupayukwa??
Vijana wa CCM na Upinzani jifunzeni siasa za kistaarabu!!Mtatuharibia nchi