The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
ACHANA na ufundi wake uwanjani. Hii ya sasa ni kali zaidi na nyota wa Yanga raia wa Ivory Coast kazua balaa jipya kwa wasanii wa kike wa Bongo Fleva na Bongo Movie ikiwa ni siku chache tu tangu Stephanie Aziz Ki kuangukia kwa mjasiriamali, Hamisa Mobetto na kuamua kufunga ndoa.
Pacome amekuwa na ushawishi mkubwa kwa wanawake wengi mjini na baadhi kuzushiwa kutoka naye kimapenzi huku wakikataa na kudai ni marafiki tu, lakini kwa kinachoendelea haitashangaza yakitokea kama yaliyotokea kwa Aziz Ki.
Hii ni baada ya wasanii hao kuonyesha wazi wanamzimikia nyota huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga anayefanya vizuri na klabu hiyo na kwa nyakati tofauti wamefunguka kumhusu bila kuficha hisia zao kwake wakiwemo mastaa Wema Sepetu na Gigy Money.
Wasanii hao ambao ni mashabiki wa klabu hiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wakibeba kombe hilo mara tatu mfululizo, walimzungumzia kiungo huyo mshambuliaji aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast na hapa wanafunguka ni jinsi gani wanamkubali.
Wema Sepetu
"Mimi ni shabiki wa Yanga, japo siwezi taja majina ya timu zote sababu siwafuatilii sana, ila ukiniuliza mchezaji gani ananikosha akiwa uwanjani nitakwambia Pacome. Napenda jinsi anavyojituma uwanjani, yaani anapambana, pia anamuonekano mzuri hata akiwa nje ya uwanja, ukimuangalia tu, unasema yes huyu ni bonge la mchezaji."
Gigy Money
"Yule Pacome Zouzoua namzimikia sana, kwanza mimi sijui mpira ila nikisikia siku Yanga inacheza, basi namwangalia Pacome tu atafanya nini uwanjani. Yule bana ana kitu halafu smart boy na anajua wajibu wake, we angalia vizuri jina lake linavyowika ukiona hivyo basi ana kazi nzuri uwanjani, mie nampenda sana."