Wema sepetu anasakwa na polisi baada ya kumtukana meneja wa hoteli wakati pombe ikiwa utosini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI POMBE IKIWA UTOSINI


DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.



Akizungumza na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.

Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki zake walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.


Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.


Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.

Aliongeza kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.


"Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni."

Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO


WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI POMBE IKIWA UTOSINI - MPEKUZI HURU
 
Who said she cant manage THEM ALLL!! I think th girl is good with polisiCCM, cause they will easily foll n LOVE!!
 
kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu
hii kali, dume unapigwa makofi na wema kwenye eneo lako bila kumlamba kichwa kimoja tu, ukamvalisha sura ya gendaeka akaringe nayo bongo movie?
 
Wema umalaya umezidi hafai hata kwenye hii jamii sasa.
 
hii kali, dume unapigwa makofi na wema kwenye eneo lako bila kumlamba kichwa kimoja tu, ukamvalisha sura ya gendaeka akaringe nayo bongo movie?

Hapo sasa unaitafuta jela na hakuna atakayekuonea huruma...umpige mwanamke, mbele ya adhara, tena mwanamke maarufu! Muulize T.I.D ajua utamu wa kupiga watu.
 
eti diva, jaman mpotezeeni tu hela znyw hatujui amezipatia wapi
 
Hapo sasa unaitafuta jela na hakuna atakayekuonea huruma...umpige mwanamke, mbele ya adhara, tena mwanamke maarufu! Muulize T.I.D ajua utamu wa kupiga watu.

Akikunasa vibao katika eneo lako uweza kumpa pigo moja la nguvu, na ukashinda kesi.
 
Akikunasa vibao katika eneo lako uweza kumpa pigo moja la nguvu, na ukashinda kesi.

How!? self defence? mwanaume useme self defence dhidi ya mwanamke hasiye hata na silaha!?
 
How!? self defence? mwanaume useme self defence dhidi ya mwanamke hasiye hata na silaha!?

sio self defence, nimesahau wanaitaje, ni kwamba mtu anapokushtukiza kukushambulia automatically brain yako na mwili wako vita react ku fight back haraka sana, na kuna muda unatakiwa usipite, inatakiwa in less than two seconds uwe ume react tayari, baada ya sekunde mbili wana assume akili ya kawaida inakua ishakurudia hivyo kosa linaweza kuwa lako.
 
Jeuri ya fedha hyo....Manager mzima na mambupu yako unapigwa makofi na wema? Ha ha ha ha yani ni kama yule askari wa mliman city aliyepigwa akapasuliwa uso na ben kinyaia.
 
hivi karibuni nilisikia kwenye "u heard" ya Sudi Brown wa Clouds FM mtu kama meneja wa hotel akikiri Wema alimshambulia!
 
Nafikiri kesi yake iwe kama ya T.I.D ili ajifunze adabu, akakae jela mwaka akirudi atakuwa kanyooka. ------- zake.
 
Huyo wema mbeba unga mkubwa hapa tz na huyo basha wake dimnd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…