Binti Sepetu kama unaingia humu, tafadhali usituaibishe wanawake wenzio.Pls spare us this time.
Ushauri wa bure : tafuta ukarabati wa tabia kwanza kisha ujipange kwa 2025! Utakuwa umekomaa kimaisha na kisiasa labda.Tuombe uzima.
Katika kujipanga, anza kujishughulisha na huduma za kijamii, ongeza shule, jiepushe na makundi mabaya,tulia usijiingize tena katika mahusiano yenye utata na watu watata. Maliza kesi zako ikiwezekana nje ya mahakama (hili laweza kuwa gumu kama kesi ishaanza kusikilizwa) au subiri kesi iishe na ukubali matokeo.Kama ni kifungo basi tumikia kifungo na uwe na mfano mzuri ukiwa jela ( god forbid!).
Tafuta mentors watakaokuwa wanakupa ushauri na miongozo yamaisha na career ya siasa kama uko serious.
Kila la kheri!